Isaya 64:6-9
Isaya 64:6-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Sote tumekuwa kama watu walio najisi; matendo yetu yote mema ni kama nguo chafu. Sote tunanyauka kama majani, uovu wetu watupeperusha kama upepo. Hakuna hata mmoja anayekuja kukuomba; hakuna anayejishughulisha kukutafuta. Wewe unauficha uso wako mbali nasi, umetuacha tukumbwe na maovu yetu. Hata hivyo, ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni Baba yetu. Sisi ni kama udongo, wewe ni mfinyanzi. Sisi sote ni kazi ya mikono yako. Usitukasirikie mno, ee Mwenyezi-Mungu, usiukumbuke uovu wetu daima! Ukumbuke kwamba sisi sote ni watu wako!
Isaya 64:6-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo. Tena hapana aliitiaye jina lako, ajitahidiye akushike; kwa kuwa umetuficha uso wako, nawe umetukomesha kwa njia ya maovu yetu. Lakini sasa, Ee BWANA, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako. Ee BWANA, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu wako.
Isaya 64:6-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo. Tena hapana aliitiaye jina lako, ajitahidiye akushike; kwa kuwa umetuficha uso wako, nawe umetukomesha kwa njia ya maovu yetu. Lakini sasa, Ee BWANA, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako. Ee BWANA, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu wako.
Isaya 64:6-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Sisi sote tumekuwa kama mtu aliye najisi, nayo matendo yetu yote ya uadilifu ni kama matambaa machafu; sisi sote tunasinyaa kama jani, na kama upepo maovu yetu hutupeperusha. Hakuna yeyote anayeliitia jina lako wala anayejitahidi kukushika, kwa kuwa umetuficha uso wako na kutuacha tudhoofike kwa sababu ya dhambi zetu. Lakini, Ee BWANA, wewe ndiwe Baba yetu. Sisi ni udongo, na wewe ndiwe mfinyanzi; sisi sote tu kazi ya mkono wako. Ee BWANA, usikasirike kupita kiasi, usizikumbuke dhambi zetu milele. Ee Bwana, utuangalie, twakuomba, kwa kuwa sisi sote tu watu wako.