Isaya 64:4-5
Isaya 64:4-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Tangu kale hakuna aliyepata kuona wala kusikia kwa masikio yake; hakuna aliyepata kumwona Mungu aliye kama wewe atendaye mambo kwa ajili ya wale wanaomtegemea! Wewe waja kuwasaidia watendao haki kwa furaha, wanaokukumbuka na kuzingatia njia zako. Ulitukasirikia tulipokuwa wenye dhambi; sisi tumeasi kwa muda mrefu.
Isaya 64:4-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana tangu zamani za kale watu hawakusikia, wala kufahamu kwa masikio, wala jicho halikuona Mungu, ila wewe, atendaye mambo kwa ajili yake amngojaye. Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika dhambi kwa muda mrefu, nasi Je! Tutaokolewa?
Isaya 64:4-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana tangu zamani za kale watu hawakusikia, wala kufahamu kwa masikio, wala jicho halikuona Mungu, ila wewe, atendaye mambo kwa ajili yake amngojaye. Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika mambo haya muda mwingi; nasi, je! Tutaokolewa?
Isaya 64:4-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Tangu nyakati za zamani hakuna yeyote aliyesikia, hakuna sikio lililotambua, hakuna jicho lililomwona Mungu mwingine ila wewe, anayetenda mambo kwa ajili ya wale wamngojeao. Uliwasaidia watu wale watendao yaliyo haki kwa furaha, wale wazikumbukao njia zako. Lakini wakati tulipoendelea kutenda dhambi kinyume na njia zako, ulikasirika. Tutawezaje basi kuokolewa?