Isaya 64:10-12
Isaya 64:10-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Miji yako mitakatifu imekuwa nyika; Siyoni umekuwa mahame, Yerusalemu umekuwa uharibifu. Nyumba yetu takatifu na nzuri, ambamo wazee wetu walikusifu, imeteketezwa kwa moto. Mahali petu pote pazuri pamekuwa magofu. Je, kwa hayo yote utajizuia usifanye kitu? Je, utaendelea kunyamaza tu, ee Mwenyezi-Mungu, na kututesa kupita kiasi?
Isaya 64:10-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Miji yako mitakatifu imekuwa jangwa, Sayuni umekuwa jangwa, Yerusalemu umekuwa ukiwa. Nyumba yetu takatifu, nzuri, walimokusifu baba zetu, imeteketea moto; vitu vyetu vyote vyenye kupendeza vimeharibika. Utajizuia usiyaangalie mambo haya, Ee BWANA? Utanyamaza, na kutuadhibu vikali?
Isaya 64:10-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Miji yako mitakatifu imekuwa jangwa, Sayuni umekuwa jangwa, Yerusalemu umekuwa ukiwa. Nyumba yetu takatifu, nzuri, walimokusifu baba zetu, imeteketea moto; vitu vyetu vyote vyenye kupendeza vimeharibika. Utajizuia usiyaangalie mambo haya, Ee BWANA? Utanyamaza, na kututesa sana?
Isaya 64:10-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Miji yako mitakatifu imekuwa jangwa; hata Sayuni ni jangwa, Yerusalemu ni ukiwa. Hekalu letu takatifu na tukufu, ambako baba zetu walikusifu wewe, limechomwa kwa moto, navyo vitu vyote tulivyovithamini vimeharibika. Ee BWANA, baada ya haya yote, utajizuia? Je, utanyamaza, na kutuadhibu kupita kiasi?