Isaya 64:1-5
Isaya 64:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Laiti ungalizipasua mbingu ukashuka chini, milima ikakuona na kutetemeka kwa hofu! Ingeteketea kama moto uchomavyo kichaka, kama vile moto uchemshavyo maji. Njoo upate kuwajulisha maadui zako jina lako nayo mataifa yatetemeke kwa kuwako kwako! Wakati ulipotenda maajabu ambayo hatukutazamia, ulishuka chini nayo milima ikatetemeka ilipokuona. Tangu kale hakuna aliyepata kuona wala kusikia kwa masikio yake; hakuna aliyepata kumwona Mungu aliye kama wewe atendaye mambo kwa ajili ya wale wanaomtegemea! Wewe waja kuwasaidia watendao haki kwa furaha, wanaokukumbuka na kuzingatia njia zako. Ulitukasirikia tulipokuwa wenye dhambi; sisi tumeasi kwa muda mrefu.
Isaya 64:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Laiti ungepasua mbingu, na kushuka, ili milima itetemeke mbele zako; kama vile moto uchomapo vichaka, na moto uchemshapo maji; ili kuwajulisha adui zako jina lako, mataifa wakatetemeke mbele zako! Ulipofanya mambo ya kutisha tusiyoyatazamia, ulishuka, milima ikatetemeka mbele zako. Maana tangu zamani za kale watu hawakusikia, wala kufahamu kwa masikio, wala jicho halikuona Mungu, ila wewe, atendaye mambo kwa ajili yake amngojaye. Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika dhambi kwa muda mrefu, nasi Je! Tutaokolewa?
Isaya 64:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Laiti ungepasua mbingu, na kushuka, ili milima iteteme mbele zako; kama vile moto uchomapo vichaka, na moto uchemshapo maji; ili kuwajulisha adui zako jina lako, mataifa wakatetemeke mbele zako! Ulipofanya mambo ya kutisha tusiyoyatazamia, ulishuka, milima ikatetema mbele zako. Maana tangu zamani za kale watu hawakusikia, wala kufahamu kwa masikio, wala jicho halikuona Mungu, ila wewe, atendaye mambo kwa ajili yake amngojaye. Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika mambo haya muda mwingi; nasi, je! Tutaokolewa?
Isaya 64:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Laiti ungepasua mbingu na kushuka chini, ili milima itetemeke mbele zako! Kama vile moto unavyoteketeza vijiti na kusababisha maji kuchemka, shuka ukafanye jina lako lijulikane kwa adui zako, na kusababisha mataifa yatetemeke mbele zako! Kwa maana ulipofanya mambo ya kutisha ambayo hatukuyatazamia, ulishuka, nayo milima ikatetemeka mbele zako. Tangu nyakati za zamani hakuna yeyote aliyesikia, hakuna sikio lililotambua, hakuna jicho lililomwona Mungu mwingine ila wewe, anayetenda mambo kwa ajili ya wale wamngojeao. Uliwasaidia watu wale watendao yaliyo haki kwa furaha, wale wazikumbukao njia zako. Lakini wakati tulipoendelea kutenda dhambi kinyume na njia zako, ulikasirika. Tutawezaje basi kuokolewa?