Isaya 62:11-12
Isaya 62:11-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu ametangaza duniani kote, waambie watu wa Siyoni: “Mkombozi wenu anakuja, zawadi yake iko pamoja naye na tuzo lake liko mbele yake.” Nyinyi mtaitwa: “Watu Watakatifu”, “Watu waliokombolewa na Mwenyezi-Mungu.” Na Yerusalemu utaitwa: “Mji aupendao Mungu”, “Mji ambao Mungu hakuuacha.”
Isaya 62:11-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tazama, BWANA ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia, Mwambieni binti Sayuni, Tazama, wokovu wako unakuja; Tazama, thawabu yake iko pamoja naye, Na malipo yake yako mbele zake. Nao watawaita, Watu watakatifu, Waliokombolewa na BWANA; Nawe utaitwa, Aliyetafutwa, Mji usioachwa.
Isaya 62:11-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tazama, BWANA ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia, Mwambieni binti Sayuni, Tazama, wokovu wako unakuja; Tazama, thawabu yake i pamoja naye, Na malipo yake yako mbele zake. Nao watawaita, Watu watakatifu, Waliokombolewa na BWANA; Nawe utaitwa, Aliyetafutwa, Mji usioachwa.
Isaya 62:11-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA ametoa tangazo hadi miisho ya dunia: “Mwambie Binti Sayuni, ‘Tazama, mwokozi wako anakuja! Tazama ujira wake uko pamoja naye, na malipo yake yanafuatana naye!’ ” Wataitwa Watu Watakatifu, Waliokombolewa na BWANA; nawe utaitwa Aliyetafutwa, Mji Usioachwa Tena.