Isaya 60:1-3
Isaya 60:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Inuka ee Siyoni uangaze; maana mwanga unachomoza kwa ajili yako, utukufu wa Mwenyezi-Mungu unakuangaza. Tazama, giza litaifunika dunia, giza nene litayafunika mataifa; lakini wewe, Mwenyezi-Mungu atakuangazia, utukufu wake utaonekana kwako. Mataifa yataujia mwanga wako, wafalme waujia mwanga wa pambazuko lako.
Isaya 60:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa BWANA umekuzukia. Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika makabila ya watu; Bali BWANA atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako. Na mataifa wataijia nuru yako, Na wafalme kuujia mwanga wa mapambazuko yako.
Isaya 60:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa BWANA umekuzukia. Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali BWANA atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako. Na mataifa wataijilia nuru yako, Na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako.
Isaya 60:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja na utukufu wa BWANA umezuka juu yako. Tazama, giza litaifunika dunia, na giza nene litayafunika mataifa, lakini BWANA atazuka juu yako na utukufu wake utaonekana juu yako. Mataifa watakuja kwenye nuru yako na wafalme kwa mwanga wa mapambazuko yako.