Isaya 51:21-23
Isaya 51:21-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Basi, sikiliza ewe Yerusalemu unayeteseka; sikiliza wewe uliyelewa, lakini sio kwa divai. Bwana, Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi: “Nimekuondolea kikombe cha kuyumbisha, hutakunywa tena kikombe cha ghadhabu yangu. Nitawanywesha watesi wako kikombe hicho waliokuambia ulale chini wapite juu yako; wakaufanya mgongo wako kama ardhi, kama barabara yao ya kupitia.”
Isaya 51:21-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi, kwa sababu ya hayo, ulisikilize neno hili, ewe uliyeteswa, na kulewa, lakini si kwa mvinyo; BWANA, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevyalevya, hilo bakuli la hasira yangu; hutalinywea tena; nami nitalitia mikononi mwao wakutesao; waliokuambia nafsi yako, Inama, tupate kupita; nawe uliufanya mgongo wako kuwa kama nchi, na kama njia, kwa hao wapitao juu yake.
Isaya 51:21-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi, kwa sababu ya hayo, ulisikilize neno hili, ewe uliyeteswa, na kulewa, lakini si kwa mvinyo; BWANA, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevya-levya, hilo bakuli la kikombe cha hasira yangu; hutakinywea tena; nami nitakitia mikononi mwao wakutesao; waliokuambia nafsi yako, Inama, tupate kupita; nawe uliufanya mgongo wako kuwa kama nchi, na kama njia, kwa hao wapitao juu yake.
Isaya 51:21-23 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa hiyo sikiliza hili, wewe uliyeteswa, uliyelewa, lakini si kwa mvinyo. Hili ndilo asemalo BWANA Mwenyezi wako, Mungu wako, yeye ambaye huwatetea watu wake: “Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe kilichokufanya uyumbayumbe; kutoka kikombe hicho, kikombe cha kunywa cha ghadhabu yangu, kamwe hutakunywa tena. Nitakiweka mikononi mwa watesi wako, wale waliokuambia, ‘Anguka kifudifudi ili tuweze kutembea juu yako.’ Ukaufanya mgongo wako kama ardhi, kama njia yao ya kupita.”