Isaya 49:1-5
Isaya 49:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Nisikilizeni, enyi nchi za mbali, tegeni sikio, enyi watu wa mbali! Mwenyezi-Mungu aliniita kabla sijazaliwa, alitaja jina langu nikiwa tumboni mwa mama yangu. Aliyapa ukali maneno yangu kama upanga mkali, alinificha katika kivuli cha mkono wake; aliufanya ujumbe wangu mkali kama ncha ya mshale, akanificha katika podo lake. Aliniambia, “Wewe ni mtumishi wangu; kwako, Israeli, watu watanitukuza.” Lakini mimi nikafikiri, “Nimeshughulika bure, nimetumia nguvu zangu bure kabisa.” Hata hivyo, Mwenyezi-Mungu atanipa haki yangu; tuzo la kazi yangu liko kwa Mungu. Lakini asema sasa Mwenyezi-Mungu, ambaye aliniita tangu tumboni mwa mama yangu ili nipate kuwa mtumishi wake; nilirudishe taifa la Yakobo kwake, niwakusanye wazawa wa Israeli kwake. Mwenyezi-Mungu amenijalia heshima mbele yake. Mungu wangu amekuwa ndiye nguvu yangu.
Isaya 49:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nisikilizeni, enyi visiwa; tegeni masikio yenu, enyi makabila ya watu mlio mbali sana; BWANA ameniita tangu tumboni; toka tumbo la mama yangu amenitaja jina langu. Naye anifanya kinywa changu kuwa kama upanga mkali; katika kivuli cha mkono wake amenisitiri; naye amenifanya kuwa mshale uliosuguliwa; katika podo lake amenificha; akaniambia; Wewe u mtumishi wangu, Israeli, ambaye katika wewe nitatukuzwa. Lakini nikasema, Nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu yangu ina BWANA, na thawabu yangu ina Mungu wangu. Na sasa BWANA asema hivi, yeye aliyeniumba tangu tumboni niwe mtumishi wake, ili nimletee Yakobo tena, na Israeli wakusanyike mbele zake tena; (maana mimi nimepata heshima mbele ya macho ya BWANA, na Mungu wangu amekuwa nguvu zangu)
Isaya 49:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nisikilizeni, enyi visiwa; tegeni masikio yenu, enyi kabila za watu mlio mbali sana; BWANA ameniita tangu tumboni; toka tumbo la mama yangu amenitaja jina langu. Naye anifanya kinywa changu kuwa kama upanga mkali; katika kivuli cha mkono wake amenisitiri; naye amenifanya kuwa mshale uliosuguliwa; katika podo lake amenificha; akaniambia; Wewe u mtumishi wangu, Israeli, ambaye katika wewe nitatukuzwa. Lakini nikasema, Nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu yangu ina BWANA, na thawabu yangu ina Mungu wangu. Na sasa BWANA asema hivi, yeye aliyeniumba tangu tumboni niwe mtumishi wake, ili nimletee Yakobo tena, na Israeli wakusanyike mbele zake tena; (maana mimi nimepata heshima mbele ya macho ya BWANA, na Mungu wangu amekuwa nguvu zangu)
Isaya 49:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nisikilizeni, enyi visiwa, sikieni hili, ninyi mataifa mlio mbali: Kabla sijazaliwa, BWANA aliniita, tangu kuzaliwa kwangu, amelitaja jina langu. Akafanya kinywa changu kuwa kama upanga ulionolewa, katika uvuli wa mkono wake akanificha; akanifanya kuwa mshale uliosuguliwa, na kunificha katika podo lake. Akaniambia, “Wewe u mtumishi wangu, Israeli, ambaye ndani yake nitaonesha utukufu wangu.” Lakini nilisema, “Nimetumika bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida. Hata hivyo linalonistahili liko mkononi mwa BWANA, nao ujira wangu uko kwa Mungu wangu.” Sasa BWANA asema: yeye aliyeniumba tumboni kuwa mtumishi wake, kumrudisha tena Yakobo kwake na kumkusanyia Israeli, kwa maana nimepata heshima machoni pa BWANA, naye Mungu wangu amekuwa nguvu yangu