Isaya 45:4-5
Isaya 45:4-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa ajili ya mtumishi wangu Yakobo, naam, kwa ajili ya mteule wangu Israeli, nimekuita kwa jina lako; nimekupa jina la heshima ingawa wewe hunijui. “Mimi ni Mwenyezi-Mungu, wala hakuna mwingine; hakuna Mungu mwingine ila mimi. Ninakuimarisha ingawa wewe hunijui
Isaya 45:4-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa ajili ya Yakobo, mtumishi wangu, na Israeli, mteule wangu, nimekuita kwa jina lako; nimekupa jina la sifa; ijapokuwa hukunijua. Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu; nitakuimarisha ijapokuwa hukunijua
Isaya 45:4-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa ajili ya Yakobo, mtumishi wangu, na Israeli, mteule wangu, nimekuita kwa jina lako; nimekupa jina la sifa; ijapokuwa hukunijua. Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu; nitakufunga mshipi ijapokuwa hukunijua
Isaya 45:4-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa ajili ya Yakobo mtumishi wangu, Israeli niliyemchagua, nimekuita wewe kwa jina lako, na kukupa jina la heshima, ingawa wewe hunitambui. Mimi ndimi BWANA, wala hakuna mwingine, zaidi yangu hakuna Mungu. Nitakutia nguvu, ingawa wewe hujanitambua