Isaya 44:24-28
Isaya 44:24-28 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu, Mkombozi wako, aliyekuumba tangu tumboni mwa mama yako, asema: “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu niliyeumba vitu vyote. Mimi peke yangu nilizitandaza mbingu, niliiumba dunia kwa nguvu yangu mwenyewe! Mimi huzivuruga ishara za watabiri waongo na kuwapumbaza waaguzi. Mimi huyakanusha maneno ya wenye hekima na kufanya ujuzi wao kuwa upumbavu. Lakini huuthibitisha ujumbe wa mtumishi wangu, na kukamilisha maaguzi ya wajumbe wangu. Mimi ndimi niuambiaye mji wa Yerusalemu: Wewe Yerusalemu, utakaliwa tena na watu. Na miji ya Yuda: Nyinyi mtajengeka tena: Magofu yenu nitayarekebisha tena. Mimi ndimi ninayeviamuru vilindi: Kaukeni. Ndimi nimwambiaye Koreshi: Wewe utawachunga watu kwa niaba yangu. Wewe utatekeleza mipango yangu yote. Ndimi ninayesema kuhusu Yerusalemu: Wewe Yerusalemu utajengwa tena upya; na juu ya hekalu: Msingi wako utawekwa tena.”
Isaya 44:24-28 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA, mkombozi wako, yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi; Mimi ni BWANA, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke yangu; niienezaye nchi; ni nani aliye pamoja nami? Nizitanguaye ishara za waongo, na kuwatia waganga wazimu; niwarudishaye nyuma wenye hekima, na kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga; nilithibitishaye neno la mtumishi wangu, na kuyafikiliza mashauri ya wajumbe wangu; niuambiaye Yerusalemu, Utakaliwa na watu, nayo miji ya Yuda, Itajengwa, nami nitapainua mahali pake palipobomoka; niviambiaye vilindi, Kauka, nami nitaikausha mito yako; nimwambiaye Koreshi, Mchungaji wangu, naye atayatenda mapenzi yangu; hata ataunena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa.
Isaya 44:24-28 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Isaya 44:24-28 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Hili ndilo asemalo BWANA, Mkombozi wako, aliyekuumba tumboni: “Mimi ni BWANA, niliyeumba vitu vyote, niliyezitanda mbingu peke yangu, niliyeitandaza nchi mwenyewe. “Mimi huzipinga ishara za manabii wa uongo, na kuwatia upumbavu waaguzi, niyapinduaye maarifa ya wenye hekima, na kuyafanya kuwa upuzi. Mimi ndimi niyathibitishaye maneno ya watumishi wake, na kutimiza utabiri wa wajumbe wake. “Mimi ndiye niiambiaye Yerusalemu, ‘Itakaliwa na watu,’ niiambiaye miji ya Yuda kuwa, ‘Itajengwa,’ na kuhusu magofu yake, ‘Mimi nitayatengeneza,’ niiambiaye kilindi cha maji, ‘Kauka, nami nitakausha vijito vyako,’ nisemaye kuhusu Koreshi, ‘Yeye ni mchungaji wangu, naye atatimiza yote yanipendezayo; atauambia Yerusalemu, “Ukajengwe tena,” na kuhusu Hekalu, “Misingi yake na iwekwe.” ’