Isaya 42:6-7
Isaya 42:6-7 Biblia Habari Njema (BHN)
“Mimi Mwenyezi-Mungu nimekuita kutenda haki, nimekushika mkono na kukulinda. Kwa njia yako nitaweka ahadi na watu wote, wewe utakuwa mwanga wa mataifa. Utayafumbua macho ya vipofu, utawatoa wafungwa gerezani, waliokaa gizani utawaletea uhuru.
Isaya 42:6-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mimi, BWANA, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.
Isaya 42:6-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mimi, BWANA, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.
Isaya 42:6-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Mimi, BWANA, nimekuita katika haki; nitakushika mkono wako. Nitakulinda na kukufanya kuwa agano kwa ajili ya watu na nuru kwa Mataifa, kuwafungua macho wale wasioona, kuwaacha huru kutoka kifungoni wale waliofungwa, na kuwafungua kutoka gerezani wale wanaokaa gizani.