Isaya 42:17-25
Isaya 42:17-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Wote wanaotegemea sanamu za miungu, wote wanaoziambia: Nyinyi ni miungu yetu; watakomeshwa na kuaibishwa. “Sikilizeni enyi viziwi! Tazameni enyi vipofu, mpate kuona! Nani aliye kipofu ila mtumishi wangu? Nani aliye kiziwi kama mjumbe ninayemtuma? Ni nani aliye kipofu kama huyu niliyemweka wakfu, au kipofu kama mtumishi wa Mwenyezi-Mungu? Nyinyi mmeona mambo mengi, lakini hamwelewi kitu. Masikio yenu yako wazi, lakini hamsikii kitu!” Mwenyezi-Mungu, kwa ajili ya uaminifu wake, alipenda kukuza mwongozo wake na kuutukuza. Lakini hawa ni watu walioibiwa mali na kuporwa! Wote wamenaswa mashimoni, wamefungwa gerezani. Wamekuwa kama mawindo bila mtu wa kuwaokoa, wamekuwa nyara na hakuna asemaye, “Waokolewe!” Je, mtatega sikio kusikia kitu hiki? Nani kati yenu atakayesikiliza vizuri yatakayotukia? Ni nani aliyewatia Waisraeli mikononi mwa adui zao? Nani aliyewaacha wanyanganywe mali zao? Ni Mwenyezi-Mungu ambaye tumemkosea! Wazee wetu walikataa kuzifuata njia zake, wala hawakuzitii amri zake. Kwa hiyo aliwamwagia hasira yake kali, akawaacha wakumbane na vita vikali. Hasira yake iliwawakia kila upande, lakini wao hawakuelewa chochote; iliwachoma, lakini hawakutilia jambo hilo maanani.
Isaya 42:17-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Watarudishwa nyuma, wataaibishwa sana, hao wanaotumainia sanamu za mawe, na kuziambia sanamu za madini, Ninyi ndinyi miungu yetu. Sikilizeni, enyi viziwi; tazameni, enyi vipofu, mpate kuona. Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu? Au aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu, kama yeye aliye na amani? Naam, kipofu kama mtumishi wa BWANA? Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake yako wazi, lakini hasikii. BWANA akapendezwa, kwa ajili ya haki yake, kuitukuza sheria, na kuiadhimisha. Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha. Ni nani miongoni mwenu atakayetega sikio lake kuyasikia hayo? Atakayesikiliza na kusikia kwa wakati ujao? Ni nani aliyemtoa Yakobo awe mateka, aliyemtia Israeli katika mikono ya wanyang'anyi? Si yeye, BWANA? Yeye tuliyemkosea, ambaye hawakutaka kwenda katika njia zake, wala hawakuitii sheria yake. Kwa sababu hiyo alimwaga ukali wa hasira yake juu yake, na nguvu za vita; ukawasha moto wa kumzunguka pande zote, wala hakujua; ukamteketeza, wala hakuyatia hayo moyoni mwake.
Isaya 42:17-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Watarudishwa nyuma, wataaibishwa sana, hao wanaotumainia sanamu za mawe, na kuziambia sanamu za madini, Ninyi ndinyi miungu yetu. Sikilizeni, enyi viziwi; tazameni, enyi vipofu, mpate kuona. Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu? Au aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu, kama yeye aliye na amani? Naam, kipofu kama mtumishi wa BWANA? Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake ya wazi, lakini hasikii. BWANA akapendezwa, kwa ajili ya haki yake, kuitukuza sheria, na kuiadhimisha. Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha. Ni nani miongoni mwenu atakayetega sikio lake kuyasikia hayo? Atakayesikiliza na kusikia kwa wakati ujao? Ni nani aliyemtoa Yakobo awe mateka, aliyemtia Israeli katika mikono ya wanyang’anyi? Si yeye, BWANA? Yeye tuliyemkosa, ambaye hawakutaka kwenda katika njia zake, wala hawakuitii sheria yake. Kwa sababu hiyo alimwaga ukali wa hasira yake juu yake, na nguvu za vita; ukawasha moto wa kumzunguka pande zote, wala hakujua; ukamteketeza, wala hakuyatia hayo moyoni mwake.
Isaya 42:17-25 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Lakini wale wanaotumaini sanamu, wanaoviambia vinyago, ‘Ninyi ndio miungu yetu,’ watarudishwa nyuma kwa aibu kubwa. “Sikieni, enyi viziwi; tazameni, enyi vipofu, mpate kuona! Ni nani aliye kipofu isipokuwa mtumishi wangu, na kiziwi kama mjumbe ninayemtuma? Ni nani aliye kipofu kama yeye aliyejitoa kwangu, aliye kipofu kama mtumishi wa BWANA? Mmeona vitu vingi, lakini hamkuzingatia; masikio yenu yako wazi, lakini hamsikii chochote.” Ilimpendeza BWANA kwa ajili ya haki yake kufanya sheria yake kuwa kuu na tukufu. Lakini hili ni taifa lililoibwa na kutekwa nyara, wote wamenaswa katika mashimo, au wamefichwa katika magereza. Wamekuwa nyara, wala hapana yeyote awaokoaye. Wamefanywa mateka, wala hapana yeyote asemaye, “Warudishe.” Ni nani miongoni mwenu atakayesikiliza hili, au atakayezingatia kwa makini katika wakati ujao? Ni nani aliyemtoa Yakobo kuwa mateka, na Israeli kwa wateka nyara? Je, hakuwa yeye, BWANA, ambaye tumetenda dhambi dhidi yake? Kwa kuwa hawakufuata njia zake, hawakutii sheria zake. Hivyo akawamwagia hasira yake inayowaka, ukali wa vita. Iliwazunguka kwa miali ya moto, lakini hata hivyo hawakuelewa; iliwateketeza, lakini hawakuyatia moyoni.