Isaya 42:10-13
Isaya 42:10-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwimbieni Mwenyezi-Mungu wimbo mpya! Dunia yote iimbe sifa zake: Bahari na vyote vilivyomo, nchi za mbali na wakazi wake; jangwa na miji yake yote ipaaze sauti, vijiji vya wakazi wa Kedari vimsifu, wakazi wa Sela waimbe kwa shangwe; wapaaze sauti kutoka mlimani juu. Wote wakaao nchi za mbali, na wamtukuze na kumsifu Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu ajitokeza kama shujaa; kama askari vitani ajikakamua kupigana. Anapaza sauti kubwa ya vita, na kujionesha mwenye nguvu dhidi ya maadui zake.
Isaya 42:10-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Na sifa zake tokea mwisho wa dunia; Ninyi mshukao baharini, na vyote vilivyomo, Na visiwa, nao wakaao humo. Jangwa na miji yake na ipaze sauti zao, Vijiji vinavyokaliwa na Kedari; Na waimbe wenyeji wa Sela, Wapige kelele toka vilele vya milima. Na wamtukuze BWANA, Na kutangaza sifa zake visiwani. BWANA atatokea kama shujaa; Ataamsha wivu kama mtu wa vita; Atalia, naam, atapiga kelele; Atawatenda adui zake mambo makuu.
Isaya 42:10-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Na sifa zake tokea mwisho wa dunia; Ninyi mshukao baharini, na vyote vilivyomo, Na visiwa, nao wakaao humo. Jangwa na miji yake na ipaze sauti zao, Vijiji vinavyokaliwa na Kedari; Na waimbe wenyeji wa Sela, Wapige kelele toka vilele vya milima. Na wamtukuze BWANA, Na kutangaza sifa zake visiwani. BWANA atatokea kama shujaa; Ataamsha wivu kama mtu wa vita; Atalia, naam, atapiga kelele; Atawatenda adui zake mambo makuu.
Isaya 42:10-13 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mwimbieni BWANA wimbo mpya, sifa zake toka miisho ya dunia, ninyi mshukao chini baharini, na vyote vilivyomo ndani yake, enyi visiwa na wote wakaao ndani yake. Jangwa na miji yake na vipaze sauti zao; makao anamoishi Kedari na yashangilie. Watu wa Sela waimbe kwa furaha, na wapige kelele kutoka vilele vya milima. Wampe BWANA utukufu, na kutangaza sifa zake katika visiwa. BWANA ataenda kama mtu mwenye nguvu, kama shujaa atachochea shauku yake, kwa kelele ataamsha kilio cha vita, naye atashinda adui zake.