Isaya 42:1-9
Isaya 42:1-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Huyu hapa mtumishi wangu, ninayemtegemeza, mteule wangu, ninayependezwa naye; nitaweka Roho yangu juu yake, naye ataleta haki kwa mataifa. Hatapaza sauti wala kupiga kelele, wala hataipaza sauti yake barabarani. Mwanzi uliopondeka hatauvunja, na utambi unaofuka moshi hatauzima. Kwa uaminifu ataleta haki, hatazimia roho wala kukata tamaa, hadi atakaposimamisha haki juu ya dunia. Visiwa vitaweka tumaini lao katika sheria yake.” Hili ndilo asemalo Mungu, BWANA, yeye aliyeziumba mbingu na kuzitanda, aliyeitandaza dunia na vyote vinavyotoka humo, awapaye watu wake pumzi, na uzima kwa wale wanaoenda humo: “Mimi, BWANA, nimekuita katika haki; nitakushika mkono wako. Nitakulinda na kukufanya kuwa agano kwa ajili ya watu na nuru kwa Mataifa, kuwafungua macho wale wasioona, kuwaacha huru kutoka kifungoni wale waliofungwa, na kuwafungua kutoka gerezani wale wanaokaa gizani. “Mimi ndimi BWANA; hilo ndilo Jina langu! Sitampa mwingine utukufu wangu wala sanamu sifa zangu. Tazama, mambo ya kwanza yametokea, nami natangaza mambo mapya; kabla hayajatokea nawatangazia habari zake.”
Isaya 42:1-9 Biblia Habari Njema (BHN)
“Tazameni mtumishi wangu ninayemtegemeza; mteule wangu ambaye moyo wangu umependezwa naye. Nimeiweka roho yangu juu yake, naye atayaletea mataifa haki. Hatalia wala hatapiga kelele, wala hatapaza sauti yake barabarani. Mwanzi uliochubuka hatauvunja, utambi ufukao moshi hatauzima; ataleta haki kwa uaminifu. Yeye hatafifia wala kufa moyo, hata atakapoimarisha haki duniani. Watu wa mbali wanangojea mwongozo wake.” Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungu aliyeziumba mbingu, akazitandaza kama hema, yeye aliyeiunda nchi na vyote vilivyomo, yeye awapaye watu waliomo pumzi, na kuwajalia uhai wote waishio humo: “Mimi Mwenyezi-Mungu nimekuita kutenda haki, nimekushika mkono na kukulinda. Kwa njia yako nitaweka ahadi na watu wote, wewe utakuwa mwanga wa mataifa. Utayafumbua macho ya vipofu, utawatoa wafungwa gerezani, waliokaa gizani utawaletea uhuru. Jina langu mimi ni Mwenyezi-Mungu; utukufu wangu sitampa mwingine, wala sifa zangu sanamu za miungu. Tazama, mambo niliyotabiri yametukia; na sasa natangaza mambo mapya, nakueleza hayo kabla hayajatukia.”
Isaya 42:1-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu. Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu. Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; atatoa hukumu kwa uaminifu. Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake. Mungu BWANA anena, yeye aliyeziumba mbingu, na kuzitanda; yeye aliyeitandaza nchi na mazao yake; yeye awapaye pumzi watu walio juu yake; yeye awapaye roho wao waendao ndani yake. Mimi, BWANA, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa. Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu. Tazama, mambo ya kwanza yamekuwa, nami nayahubiri mambo mapya; kabla hayajatokea nawapasheni habari zake.
Isaya 42:1-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu. Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu. Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; atatokeza hukumu kwa kweli. Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake. Mungu BWANA anena, yeye aliyeziumba mbingu, na kuzitanda; yeye aliyeitandaza nchi na mazao yake; yeye awapaye pumzi watu walio juu yake; yeye awapaye roho wao waendao ndani yake. Mimi, BWANA, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa. Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu. Tazama, mambo ya kwanza yamekuwa, nami nayahubiri mambo mapya; kabla hayajatokea nawapasheni habari zake.