Isaya 40:30-31
Isaya 40:30-31 Biblia Habari Njema (BHN)
Hata vijana watafifia na kulegea; naam, wataanguka kwa uchovu. Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu, watapata nguvu mpya. Watapanda juu kwa mabawa kama tai; watakimbia bila kuchoka; watatembea bila kulegea.
Isaya 40:30-31 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hata vijana watazimia na kuchoka, na vijana wanaume wataanguka; bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Isaya 40:30-31 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Isaya 40:30-31 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hata vijana huchoka na kulegea, nao vijana wanaume hujikwaa na kuanguka, bali wale wamtumainio BWANA atafanya upya nguvu zao. Watapaa juu kwa mabawa kama tai; watapiga mbio wala hawatachoka, watatembea kwa miguu wala hawatazimia.