Isaya 40:3-5
Isaya 40:3-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Sauti ya mtu anaita jangwani: “Mtayarishieni Mwenyezi-Mungu njia, nyosheni barabara kuu kwa ajili ya Mungu wetu. Kila bonde litasawazishwa, kila mlima na kilima vitashushwa; ardhi isiyo sawa itafanywa sawa, mahali pa kuparuza patalainishwa. Kisha utukufu wa Mwenyezi-Mungu utafunuliwa, na watu wote pamoja watauona. Mwenyezi-Mungu mwenyewe ametamka hayo.”
Isaya 40:3-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya BWANA; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu. Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipoinuka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patasawazishwa; Na utukufu wa BWANA utafunuliwa, Na watu wote watauona pamoja; Kwa kuwa kinywa cha BWANA kimenena haya.
Isaya 40:3-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya BWANA; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu. Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patasawazishwa; Na utukufu wa BWANA utafunuliwa, Na wote wenye mwili watauona pamoja; Kwa kuwa kinywa cha BWANA kimenena haya.
Isaya 40:3-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Sauti ya mtu aliaye nyikani: “Itengenezeni njia ya BWANA jangwani, yanyoosheni mapito nyikani kwa ajili ya Mungu wetu. Kila bonde litainuliwa, kila mlima na kilima kitashushwa; penye mabonde patanyooshwa, napo palipoparuza patasawazishwa. Utukufu wa BWANA utafunuliwa, nao wanadamu wote watauona pamoja. Kwa maana kinywa cha BWANA kimenena.”