Isaya 40:13-14 - Compare All Versions
Isaya 40:13-14 BHN (Biblia Habari Njema)
Nani awezaye kuiongoza akili ya Mwenyezi-Mungu, au kuwa mshauri wake na kumfunza? Mwenyezi-Mungu alimtaka nani shauri, ndipo akapata kuwa mwenye ujuzi? Nani aliyemfunza njia za haki? Nani aliyemfundisha maarifa, na kumwonesha namna ya kuwa na akili?
Isaya 40:13-14 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni nani aliyemwongoza roho ya BWANA, na kumfundisha kwa kuwa mshauri wake? Alifanya shauri na nani, ni nani aliyemwelimisha na kumfunza njia ya hukumu, na kumfunza maarifa, na kumwonyesha njia ya fahamu?
Isaya 40:13-14 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Ni nani aliyemwongoza Roho ya BWANA, na kumfundisha kwa kuwa mshauri wake? Alifanya shauri na nani, ni nani aliyemwelimisha na kumfunza njia ya hukumu, na kumfunza maarifa, na kumwonesha njia ya fahamu?
Isaya 40:13-14 NEN (Neno)
Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya BWANA, au kumfundisha akiwa kama mshauri wake? Ni nani ambaye BWANA ametaka shauri kwake ili kumwelimisha, naye ni nani aliyemfundisha njia iliyo sawa? Ni nani aliyemfundisha maarifa au kumwonesha mapito ya ufahamu?