Isaya 40:1-3
Isaya 40:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu wenu asema: “Wafarijini watu wangu, nendeni mkawafariji. Semeni na wenyeji wa Yerusalemu kwa upole, waambieni kwamba utumwa wao umekwisha, wamesamehewa uovu wao. Mwenyezi-Mungu amewaadhibu maradufu kwa sababu ya dhambi zao zote.” Sauti ya mtu anaita jangwani: “Mtayarishieni Mwenyezi-Mungu njia, nyosheni barabara kuu kwa ajili ya Mungu wetu.
Isaya 40:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu. Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa dhambi zake zote. Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya BWANA; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu.
Isaya 40:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu. Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa dhambi zake zote. Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya BWANA; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu.
Isaya 40:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wafarijini, wafarijini watu wangu, asema Mungu wenu. Sema na Yerusalemu kwa upole, umtangazie kwamba kazi yake ngumu imekamilika, kwamba dhambi yake imelipiwa fidia, kwamba amepokea kutoka mkononi mwa BWANA maradufu kwa ajili ya dhambi zake zote. Sauti ya mtu aliaye nyikani: “Itengenezeni njia ya BWANA jangwani, yanyoosheni mapito nyikani kwa ajili ya Mungu wetu.