Isaya 38:18-20
Isaya 38:18-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Huko kuzimu mtu hawezi kukushukuru wewe; waliokufa hawawezi kukushukuru wewe. Wala washukao huko shimoni hawawezi tena kutumainia uaminifu wako. Walio hai ndio wanaokushukuru, kama na mimi ninavyofanya leo. Kina baba huwajulisha watoto wao uaminifu wako. “Mwenyezi-Mungu ataniokoa. Nasi tutamsifu kwa nyimbo za vinubi siku zote za maisha yetu, nyumbani kwake Mwenyezi-Mungu.”
Isaya 38:18-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; Wale washukao shimoni hawawezi kuutumainia uaminifu wako. Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo; Baba atawajulisha watoto uaminifu wako. BWANA yu tayari kunipa wokovu. Basi, kwa vinubi tutaziimba nyimbo zangu, Siku zote za maisha yetu nyumbani mwa BWANA.
Isaya 38:18-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; Wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako. Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo; Baba atawajulisha watoto kweli yako. BWANA yu tayari kunipa wokovu. Basi, kwa vinubi tutaziimba nyimbo zangu, Siku zote za maisha yetu nyumbani mwa BWANA.
Isaya 38:18-20 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa maana kaburi haliwezi kukusifu, mauti haiwezi kuimba sifa zako; wale wanaoshuka shimoni hawawezi kuutarajia uaminifu wako. Walio hai, walio hai: hao wanakusifu, kama ninavyofanya leo. Baba huwaambia watoto wao habari za uaminifu wako. BWANA ataniokoa, nasi tutaimba kwa vyombo vya nyuzi siku zote za maisha yetu katika Hekalu la BWANA.