Isaya 36:1-2
Isaya 36:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Mnamo mwaka wa kumi na nne wa utawala wa mfalme Hezekia, mfalme Senakeribu wa Ashuru aliishambulia miji yote yenye ngome ya Yuda na kuiteka. Kisha mfalme wa Ashuru alimtuma jemadari mkuu kutoka Lakishi na jeshi kubwa kumwendea mfalme Hezekia. Jemadari alisimama karibu na mfereji wa bwawa lililoko upande wa juu katika barabara kuu inayoelekea uwanda wa Dobi.
Isaya 36:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikawa, katika mwaka wa kumi na nne wa kutawala kwake mfalme Hezekia, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akapanda ili kupigana na miji yote ya Yuda yenye boma, akaitwaa. Mfalme wa Ashuru akamtuma amiri toka Lakishi pamoja na jeshi kubwa kwenda hadi Yerusalemu kwa mfalme Hezekia. Naye akasimama karibu na mfereji wa bwawa la juu, lililo katika njia kuu ya kuuendea Uwanda wa Dobi.
Isaya 36:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikawa, katika mwaka wa kumi na nne wa kumiliki kwake mfalme Hezekia, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akapanda ili kupigana na miji yote ya Yuda yenye boma, akaitwaa. Mfalme wa Ashuru akamtuma amiri toka Lakishi hata Yerusalemu, kwa mfalme Hezekia, pamoja na jeshi kubwa. Naye akasimama karibu na mfereji wa birika ya juu, iliyo katika njia kuu ya kuuendea uwanda wa dobi.
Isaya 36:1-2 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Katika mwaka wa kumi na nne wa utawala wa Mfalme Hezekia, Senakeribu mfalme wa Ashuru akaishambulia miji yote ya Yuda yenye ngome na kuiteka. Kisha mfalme wa Ashuru akamtuma jemadari wa jeshi pamoja na jeshi kubwa kutoka Lakishi hadi kwa Mfalme Hezekia huko Yerusalemu. Jemadari wa jeshi akasimama kwenye mfereji wa Bwawa la Juu, lililojengwa katika barabara iendayo kwenye Uwanja wa Dobi.