Isaya 27:11 - Compare All Versions
Isaya 27:11 BHN (Biblia Habari Njema)
Matawi ya miti yamekauka na kuvunjika; kina mama huyaokota wakawashia moto. Watu hawa hawajaelewa kitu, kwa hiyo Mungu, Muumba wao, hatawahurumia, yeye aliyewafanya, hatawafadhili.
Isaya 27:11 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.
Isaya 27:11 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.
Isaya 27:11 NEN (Neno)
Wakati vijiti vyake vimekauka, huvunjwa nao wanawake huja na kuwasha navyo moto. Kwa kuwa hili ni taifa lisilo na ufahamu, kwa hiyo yeye aliyewafanya hana huruma juu yao, Muumba wao hawaoneshi fadhili.