Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 23:1-18

Isaya 23:1-18 Biblia Habari Njema (BHN)

Kauli ya Mungu dhidi ya Tiro. Ombolezeni, enyi mabaharia wa mbali baharini, maana Tiro mji wenu umeharibiwa, humo hamna tena makao wala bandari. Mtazipokea habari hizo mtakaporejea kutoka Kupro. Nyamazeni kwa mshangao enyi wakazi wa pwani, naam, tulieni enyi wafanyabiashara wa Sidoni, ambao wajumbe wenu wanapita baharini, wakasafiri katika bahari nyingi. Mapato yenu yalikuwa nafaka ya Misri, mkaweza kufanya biashara na mataifa. Aibu kwako ewe Sidoni, mji wa ngome kando ya bahari! Bahari yenyewe yatangaza: “Sijapata kuwa na uchungu wa kuzaa, wala sijawahi kuzaa; sijawahi kulea wavulana, wala kutunza wasichana!” Habari zitakapoifikia Misri kwamba Tiro imeangamizwa, Wamisri watafadhaika sana. Ombolezeni enyi wenyeji wa Foinike! Jaribuni kukimbilia Tarshishi. Je, huu ndio mji wa furaha wa Tiro, mji ambao ulijengwa zamani za kale, ambao wakazi wake walikwenda kumiliki nchi za mbali? Ni nani aliyepanga mambo haya dhidi ya Tiro, mji uliowatawaza wafalme, wafanyabiashara wake walikuwa wakuu, wakaheshimiwa duniani kote? Ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi! Yeye ndiye aliyeyapanga haya yote. Alifanya hivyo akiharibu kiburi chao na kuwaaibisha waheshimiwa wake. Limeni sasa ardhi yenu enyi wakazi wa Tarshishi; maana hamna tena bandari kwa ajili ya meli kubwa. Mwenyezi-Mungu ameunyosha mkono wake juu ya bahari, amezitetemesha falme; ametoa amri kuziharibu ngome za Kanaani. Alisema: “Ewe binti Sidoni hutaweza kufanya sherehe tena; hata ukikimbilia Kupro, huko nako hutapata pumziko!” (Ni Wakaldayo, wala si Waashuru, waliowaacha wanyama wa porini wauvamie mji wa Tiro. Wao ndio waliouzungushia mji huo minara ya kuushambulia, wakayabomoa majumba yake na kuufanya magofu.) Pigeni yowe enyi meli za Tarshishi, maana kimbilio lenu limeharibiwa. Hapo mji wa Tiro utasahaulika kwa muda wa miaka sabini, muda wa maisha ya mfalme. Baada ya miaka hiyo sabini, mji wa Tiro utakumbwa na kile watu wanachoimba juu ya malaya: “Twaa kinubi chako uzungukezunguke mjini, ewe malaya uliyesahaulika! Imba nyimbo tamutamu. Imba nyimbo nyinginyingi ili upate kukumbukwa tena.” Baada ya miaka hiyo sabini, Mwenyezi-Mungu atauadhibu mji wa Tiro, nao utarudia kufanya uzinzi kwa kujiuza kwa mataifa yote ya dunia. Fedha utakayopata itawekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Mji wenyewe hautafaidika kwa fedha hiyo ila wale wanaomwabudu Mwenyezi-Mungu wataitumia kununulia chakula kingi na mavazi mazuri.

Shirikisha
Soma Isaya 23

Isaya 23:1-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Ufunuo juu ya Tiro. Toeni sauti za uchungu, enyi merikebu za Tarshishi, kwa maana umeharibika kabisa, hata hapana nyumba, hapana mahali pa kuingia; toka nchi ya Kitimu wamefunuliwa habari. Tulieni, enyi mkaao kisiwani; wewe ambaye wafanya biashara wa Sidoni, wavukao bahari, walikujaza. Vitu vilivyopandwa, vya Shihori, mavuno ya Nile, yaliyokuja juu ya maji mengi, ndilo pato lake, naye alikuwa soko la mataifa. Tahayari, Ee Sidoni; kwa maana bahari imenena, hiyo ngome ya bahari ilisema, Sikuona uchungu, wala sikuzaa, wala sikulea vijana, wala sikulea wanawali. Habari itakapofika Misri wataona uchungu sana kwa sababu ya habari ya Tiro. Piteni mpaka Tarshishi, enyi mkaao kisiwani, toeni sauti ya uchungu. Je! Huu ndio mji wenu wa furaha, ambao mwanzo wake ulikuwako tangu siku za kale, ambao miguu yake ilimchukua akae mbali sana? Ni nani aliyefanya shauri hili juu ya Tiro, uliotia watu mataji, ambao wafanya biashara wake walikuwa wana wa wafalme, na wachuuzi wake ni watu wakuu wa dunia? BWANA wa majeshi ndiye aliyefanya shauri hili, ili kuharibu kiburi cha utukufu wote, na kuwaaibisha watu wa duniani wote pia. Pita katika nchi yako, kama Nile, Ee binti wa Tarshishi, hapana tena mshipi wa kukuzuia. Amenyosha mkono wake juu ya bahari, amezitikisa falme; Bwana ametoa amri katika habari za Kanaani, kuziangamiza ngome zake. Naye akasema, Usizidi kufurahi, ewe bikira uliyeaibishwa, binti wa Sidoni, haya, ondoka, uende hadi Kitimu; huko nako hutapata raha. Tazama, nchi ya Wakaldayo; watu hao hawako tena; Mwashuri ameiweka tayari kwa hayawani wa jangwani; wamesimamisha ngome zao za vita, wameyaharibu majumba yake ya enzi, akaufanya kuwa uharibifu. Pigeni yowe, enyi merikebu za Tarshishi; maana ngome yenu imefanywa ukiwa. Basi, itakuwa katika siku ile, Tiro utasahauliwa miaka sabini, kadiri ya siku za mfalme mmoja; hata mwisho wa miaka sabini, Tiro utakuwa kama vile ulivyo wimbo wa kahaba. Twaa kinubi, tembea mjini, Ewe kahaba uliyesahauliwa; Piga vizuri, imba nyimbo nyingi, Upate kukumbukwa tena. Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, BWANA ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia. Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.

Shirikisha
Soma Isaya 23

Isaya 23:1-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Ufunuo juu ya Tiro. Toeni sauti za uchungu, enyi merikebu za Tarshishi, kwa maana umeharibika kabisa, hata hapana nyumba, hapana mahali pa kuingia; toka nchi ya Kitimu wamefunuliwa habari. Tulieni, enyi mkaao kisiwani; wewe ambaye wafanya biashara wa Sidoni, wavukao bahari, walikujaza. Vitu vilivyopandwa, vya Shihori, mavuno ya Nile, yaliyokuja juu ya maji mengi, ndiyo pato lake, naye alikuwa soko la mataifa. Tahayari, Ee Sidoni; kwa maana bahari imenena, hiyo ngome ya bahari ilisema, Sikuona utungu, wala sikuzaa, wala sikulea vijana, wala sikulea wanawali. Habari itakapofika Misri wataona uchungu sana kwa sababu ya habari ya Tiro. Piteni mpaka Tarshishi, enyi mkaao kisiwani, toeni sauti ya uchungu. Je! Huu ndio mji wenu wa furaha, ambao mwanzo wake ulikuwako tangu siku za kale, ambao miguu yake ilimchukua akae mbali sana? Ni nani aliyefanya shauri hili juu ya Tiro, uliotia watu taji, ambao wafanya biashara wake walikuwa wana wa wafalme, na wachuuzi wake ni watu wakuu wa dunia? BWANA wa majeshi ndiye aliyefanya shauri hili, ili kuharibu kiburi cha utukufu wote, na kuwaaibisha watu wa duniani wote pia. Pita katika nchi yako, kama Nile, Ee binti wa Tarshishi, hapana tena mshipi wa kukuzuia. Amenyosha mkono wake juu ya bahari, amezitikisa falme; Bwana ametoa amri katika habari za Kanaani, kuziangamiza ngome zake. Naye akasema, Usizidi kufurahi, ewe bikira uliyeaibishwa, binti wa Sidoni, haya, ondoka, uende hata Kitimu; huko nako hutapata raha. Tazama, nchi ya Wakaldayo; watu hao hawako tena; Mwashuri ameiweka tayari kwa hayawani wa jangwani; wamesimamisha buruji zao za vita, wameyaharibu majumba yake ya enzi, akaufanya kuwa uharibifu. Pigeni yowe, enyi merikebu za Tarshishi; maana ngome yenu imefanywa ukiwa. Basi, itakuwa katika siku ile, Tiro utasahauliwa miaka sabini, kadiri ya siku za mfalme mmoja; hata mwisho wa miaka sabini, Tiro utakuwa kama vile ulivyo wimbo wa kahaba. Twaa kinubi, tembea mjini, Ewe kahaba uliyesahauliwa; Piga vizuri, imba nyimbo nyingi, Upate kukumbukwa tena. Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, BWANA ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia. Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.

Shirikisha
Soma Isaya 23

Isaya 23:1-18 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Neno la unabii kuhusu Tiro: Ombolezeni, enyi meli za Tarshishi! Kwa kuwa Tiro imeangamizwa, imeachwa bila nyumba wala bandari. Kuanzia nchi ya Kitimu neno limewajia. Nyamazeni kimya, enyi watu wa kisiwani, pia ninyi wafanyabiashara wa Sidoni, ambao mabaharia wamewatajirisha. Kwenye maji makuu nafaka za Shihori zilikuja; mavuno ya Mto Naili yalikuwa mapato ya Tiro, naye akawa soko la mataifa. Uaibishwe ee Sidoni, nawe ee ngome la bahari, kwa kuwa bahari imesema: “Sijapata kuwa na uchungu wa kuzaa wala sijapata kuzaa, wala sijapata kulea wana wala kutunza binti.” Habari ifikapo Misri, watakuwa katika maumivu makuu kwa ajili ya taarifa kutoka Tiro. Vukeni hadi Tarshishi, ombolezeni, enyi watu wa kisiwani. Je, huu ndio mji wenu uliojaa sherehe, mji wa zamani, zamani kabisa ambao miguu yake imeuchukua kufanya makao nchi za mbali sana? Ni nani amepanga hili dhidi ya Tiro, mji utoao mataji, ambao wafanyabiashara wake ni wana wa mfalme na wachuuzi wake ni watu mashuhuri wa dunia? BWANA wa majeshi ndiye alipanga jambo hili, ili kukishusha kiburi cha utukufu wote na kuwanyenyekeza wale wote ambao ni mashuhuri duniani. Ee Binti Tarshishi, pita katika nchi yako kama vile Mto Naili kwa kuwa huna tena bandari. BWANA amenyoosha mkono wake juu ya bahari na kuzifanya falme zake zitetemeke. Ametoa amri kuhusu Kanaani kwamba ngome zake ziangamizwe. Alisema, “Usizidi kufurahi, ee Bikira Binti Sidoni, sasa umepondwa! “Simama, vuka uende Kitimu; hata huko hutapata pumziko.” Tazama katika nchi ya Wakaldayo, watu hawa ambao sasa hawaonekani kama wapo! Waashuru wameifanya nchi hiyo kuwa mahali pa viumbe wa jangwani. Wamesimamisha minara yao ya kuuzingira, wameziteka ngome zake na kuziacha tupu na kuufanya kuwa magofu. Ombolezeni, enyi meli za Tarshishi; ngome yenu imeangamizwa! Wakati huo Tiro utasahauliwa kwa miaka sabini, muda wa maisha ya mfalme. Lakini mwisho wa miaka hiyo sabini, itakuwa kwa Tiro kama ilivyo katika wimbo wa kahaba: “Twaa kinubi, tembea mjini kote, ewe kahaba uliyesahauliwa; piga kinubi vizuri, imba nyimbo nyingi, ili upate kukumbukwa.” Mwishoni mwa miaka sabini, BWANA atatembelea Tiro. Naye Tiro atarudia ajira yake ya ukahaba, na atafanya biashara yake na falme zote duniani. Lakini faida na mapato yake yatawekwa wakfu kwa BWANA; hayatahifadhiwa wala kufichwa. Faida zake zitaenda kwa wale wanaoishi mbele za BWANA kwa ajili ya chakula tele na mavazi mazuri.

Shirikisha
Soma Isaya 23