Isaya 2:1-15
Isaya 2:1-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Neno alilopewa Isaya, mwana wa Amozi, kuhusu Yuda na Yerusalemu. Siku zijazo mlima wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu utaimarishwa kupita milima yote, utainuliwa juu ya vilima vyote. Mataifa yote yatamiminika huko, watu wengi wataujia na kusema, “Njoni tupande mlima wa Mwenyezi-Mungu, twende nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, apate kutufundisha njia zake, nasi tuishi kadiri ya mwongozo wake. Maana sheria itakuja kutoka Siyoni; neno la Mwenyezi-Mungu kutoka Yerusalemu.” Mungu atasuluhisha mizozo ya mataifa atakata mashauri ya watu wengi. Watu watafua panga za vita kuwa majembe na mikuki yao kuwa miundu ya kupogolea. Taifa halitapigana na taifa lingine wala hayatafanya tena mazoezi ya vita. Sasa, enyi wazawa wa Yakobo, njoni, tutembee katika mwanga wa Mwenyezi-Mungu. Sasa, ee Mungu, umewatupa watu wako, wazawa wa Yakobo. Maana kweli wachawi wa mashariki wamejaa kati yao, wapo na wapiga ramli kama kwa Wafilisti. Wanashirikiana na watu wageni. Nchi yao imejaa fedha na dhahabu, hazina yao ni kubwa kupindukia. Nchi yao imejaa farasi, magari yao ya kukokotwa hayana idadi. Nchi yao imejaa vinyago vya miungu, huabudu kazi ya mikono yao, vitu walivyotengeneza wao wenyewe. Kwa hiyo, kila mtu ataaibishwa na kufedheheshwa. Usiwasamehe hata kidogo, ee Mungu! Ingieni katika mwamba, mkajifiche mavumbini, kuiepa hasira ya Mwenyezi-Mungu, mbali na utukufu wa enzi yake. Siku yaja ambapo kiburi cha watu kitashushwa, majivuno ya kila mtu yatavunjwa; na Mwenyezi-Mungu peke yake atatukuzwa siku hiyo. Naam, yaja siku ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi dhidi ya wenye kiburi na majivuno, dhidi ya wote wanaojikweza; dhidi ya mierezi yote ya Lebanoni, ambayo ni mirefu na mizuri, dhidi ya mialoni yote nchini Bashani; dhidi ya milima yote mirefu, dhidi ya vilima vyote vya juu; dhidi ya minara yote mirefu, dhidi ya kuta zote za ngome
Isaya 2:1-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hili ni neno aliloliona Isaya mwana wa Amozi kuhusu Yuda na Yerusalemu. Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa BWANA, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA katika Yerusalemu. Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya BWANA. Maana wewe umewaacha watu wako, nyumba ya Israeli, kwa sababu wamejaa kawaida za mashariki, nao ni wapiga ramli kama Wafilisti, na wanapeana mikono na wana wa wageni. Tena nchi yao imejaa fedha na dhahabu, wala hapana mwisho wa hazina zao; tena nchi yao imejaa farasi, wala hapana mwisho wa magari yao. Tena nchi yao imejaa sanamu; huabudu kazi ya mikono yao, vitu vilivyotengenezwa kwa vidole vyao wenyewe. Mtu mnyonge huinama, na mtu mkubwa hujidhili; kwa hiyo usiwasamehe. Ingia ndani ya jabali; ukajifiche mavumbini mbele za utisho wa BWANA, mbele za utukufu wa enzi yake. Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye BWANA, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo. Kwa maana kutakuwa siku ya BWANA wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini. Na juu ya mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu na kuinuka, na juu ya mialoni yote ya Bashani; na juu ya milima mirefu yote, na juu ya vilima vyote vilivyoinuka; na juu ya kila mnara mrefu, na juu ya kila ukuta ulio na boma
Isaya 2:1-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hili ni neno aliloliona Isaya mwana wa Amozi katika habari za Yuda na Yerusalemu. Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa BWANA, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA katika Yerusalemu. Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya BWANA. Maana wewe umewaacha watu wako, nyumba ya Israeli, kwa sababu wamejaa kawaida za mashariki, nao ni wapiga ramli kama Wafilisti, na wanapana mikono na wana wa wageni. Tena nchi yao imejaa fedha na dhahabu, wala hapana mwisho wa hazina zao; tena nchi yao imejaa farasi, wala hapana mwisho wa magari yao. Tena nchi yao imejaa sanamu; huabudu kazi ya mikono yao, vitu vilivyofanywa kwa vidole vyao wenyewe. Mtu mnyonge huinama, na mtu mkubwa hujidhili; kwa hiyo usiwasamehe. Ingia ndani ya jabali; ukajifiche mavumbini mbele za utisho wa BWANA, mbele za utukufu wa enzi yake. Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye BWANA, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo. Kwa maana kutakuwa siku ya BWANA wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini. Na juu ya mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu na kuinuka, na juu ya mialoni yote ya Bashani; na juu ya milima mirefu yote, na juu ya vilima vyote vilivyoinuka; na juu ya kila mnara mrefu, na juu ya kila ukuta ulio na boma
Isaya 2:1-15 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hili ndilo aliloliona Isaya mwana wa Amozi kuhusu Yuda na Yerusalemu: Katika siku za mwisho mlima wa Hekalu la BWANA utaimarishwa kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote, utainuliwa juu ya vilima, na mataifa yote yatamiminika huko. Mataifa mengi yatakuja na kusema, “Njooni, twendeni kwenye mlima wa BWANA, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. Atatufundisha njia zake, ili tuweze kuenenda katika mapito yake.” Sheria itatoka Sayuni, neno la BWANA litatoka Yerusalemu. Atahukumu kati ya mataifa na ataamua migogoro ya mataifa mengi. Watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine, wala hawatajifunza vita tena. Njooni, enyi nyumba ya Yakobo, tutembeeni katika nuru ya BWANA. BWANA BWANA umewatelekeza watu wako, nyumba ya Yakobo. Wamejaa ushirikina unaotoka Mashariki, wanapiga ramli kama Wafilisti na wanashikana mikono na wapagani. Nchi yao imejaa fedha na dhahabu, hakuna mwisho wa hazina zao. Nchi yao imejaa farasi, hakuna mwisho wa magari yao ya vita. Nchi yao imejaa sanamu; wanasujudia kazi za mikono yao, vitu vile vidole vyao vimevitengeneza. Kwa hiyo mwanadamu atashushwa na binadamu atanyenyekezwa: usiwasamehe. Ingieni kwenye miamba, jificheni ardhini kutokana na utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake! Macho ya mtu mwenye majivuno yatanyenyekezwa na kiburi cha wanadamu kitashushwa, BWANA peke yake ndiye atakayetukuzwa siku hiyo. BWANA wa majeshi anayo siku aliyoiweka akiba kwa wote wenye kujivuna na wenye kiburi, kwa wote wanaojikweza (nao watanyenyekezwa), kwa mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu sana, na mialoni yote ya Bashani, kwa milima yote mirefu na vilima vyote vilivyoinuka, kwa kila mnara ulio mrefu sana na kila ukuta wenye ngome