Isaya 19:20-21
Isaya 19:20-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Madhabahu hiyo itakuwa ishara na ushuhuda kwake Mwenyezi-Mungu wa majeshi katika nchi ya Misri. Watu wakimlilia Mwenyezi-Mungu humo kwa sababu ya kukandamizwa, yeye atawapelekea mkombozi atakayewatetea na kuwakomboa. Mwenyezi-Mungu atajijulisha kwa Wamisri na hapo ndipo Wamisri watakapomkiri na kumwabudu kwa kumtolea tambiko na sadaka za kuteketezwa. Hali kadhalika, watamwekea Mwenyezi-Mungu nadhiri ambazo watazitimiza.
Isaya 19:20-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nayo itakuwa ishara na ushuhuda kwa BWANA wa majeshi katika nchi ya Misri; kwa maana watamlilia BWANA kwa sababu ya watu wawaoneao, naye atawapelekea mwokozi wa kuwatetea, naye atawaokoa. Na BWANA atajulikana na Misri, na Wamisri watamjua BWANA katika siku hiyo; naam watamtumikia kwa dhabihu na matoleo, nao watamwekea BWANA nadhiri, na kuzitekeleza.
Isaya 19:20-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nayo itakuwa ishara na ushuhuda kwa BWANA wa majeshi katika nchi ya Misri; kwa maana watamlilia BWANA kwa sababu ya watu wawaoneao, naye atawapelekea mwokozi mwenye kuwatetea, naye atawaokoa. Na BWANA atajulikana na Misri, na Wamisri watamjua BWANA katika siku hiyo; naam watamtumikia kwa dhabihu na matoleo, nao watamwekea BWANA nadhiri, na kuzitekeleza.
Isaya 19:20-21 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Itakuwa alama na ushahidi kwa ajili ya BWANA wa majeshi katika nchi ya Misri. Watakapomlilia BWANA kwa sababu ya watesi wao, Mungu atawapelekea mwokozi na mtetezi, naye atawaokoa. Hivyo BWANA atajijulisha mwenyewe kwa Wamisri, nao katika siku hiyo watamkubali BWANA. Wataabudu kwa kumtolea dhabihu na sadaka za nafaka, watamwekea BWANA nadhiri na kuzitimiza.