Isaya 18:7
Isaya 18:7 Biblia Habari Njema (BHN)
Wakati huo, Mwenyezi-Mungu wa majeshi ataletewa tambiko kutoka kwa watu warefu wenye ngozi laini, watu watishao karibu na mbali, taifa la watu wenye nguvu na ushindi, ambalo ardhi yake imegawanywa na mito. Ataletewa tambiko hizo mlimani Siyoni anapoabudiwa yeye Mwenyezi-Mungu wa majeshi.
Isaya 18:7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wakati huo BWANA wa majeshi ataletewa hidaya na watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, Ambao mito inagawanya nchi yao; Mpaka mahali pa jina la BWANA wa majeshi, mlima Sayuni.
Isaya 18:7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wakati huo BWANA wa majeshi ataletewa hedaya na watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, Ambao mito inakata nchi yao; Mpaka mahali pa jina la BWANA wa majeshi, mlima Sayuni.
Isaya 18:7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wakati huo matoleo yataletwa kwa BWANA wa majeshi kutoka kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo, kutoka kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu, kutoka taifa gomvi lenye lugha ngeni, ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito, matoleo yataletwa katika Mlima Sayuni, mahali pa Jina la BWANA wa majeshi.