Isaya 18:1-5
Isaya 18:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Ole, wake nchi iliyojaa mvumo wa mabawa, nchi iliyoko ngambo ya mito ya Kushi! Inatuma wajumbe ambao wanasafiri mtoni Nili, wamepanda mashua za mafunjo. Nendeni, enyi wajumbe wepesi, kwa taifa kubwa na hodari, la watu warefu na wa ngozi laini. Watu hao wanaoogopwa kila mahali na nchi yao imegawanywa na mito. Enyi wakazi wote ulimwenguni, nanyi mkaao duniani! Ishara itakapotolewa mlimani, tazameni! Tarumbeta itakapopigwa, sikilizeni. Maana, Mwenyezi-Mungu ameniambia hivi: “Toka makao yangu juu nitatazama yanayotukia, nimetulia kama joto katika mwanga wa jua, kama wingu la umande wakati wa mavuno. Maana, kabla ya mavuno, wakati wa kuchanua umekwisha, maua yamepukutika na kuwa zabibu mbivu, Mungu atakata chipukizi kwa kisu cha kupogolea, na kuyakwanyua matawi yanayotanda.
Isaya 18:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ole wa nchi ya uvumi wa mabawa, Iliyoko mbali kupita mito ya Kushi; Ipelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari, Na katika vyombo vya manyasi juu ya maji. Nendeni, wajumbe wepesi, kwa watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, Ambao mito inakata nchi yao. Enyi watu mkaao katika ulimwengu wote, na wenyeji wa dunia, bendera ikiinuliwa milimani, angalieni; na wakipiga tarumbeta, sikieni. Maana BWANA ameniambia hivi, Mimi nitatulia, na kuangalia katika makazi yangu, kama wakati wa mwangaza mweupe wa jua kali, mfano wa wingu la umande katika joto la mavuno. Maana kabla ya mavuno, maua yaangukapo, na maua yakawa zabibu zianzazo kuiva, ndipo atakapoyakata matawi kwa miundu, na kuviondoa vitawi vilivyopanuka na kuvikata.
Isaya 18:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ole wa nchi ya uvumi wa mabawa, Iliyoko mbali kupita mito ya Kushi; Ipelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari, Na katika vyombo vya manyasi juu ya maji. Nendeni, wajumbe wepesi, kwa watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, Ambao mito inakata nchi yao. Enyi watu mkaao katika ulimwengu wote, na wenyeji wa dunia, bendera ikiinuliwa milimani, angalieni; na wakipiga tarumbeta, sikieni. Maana BWANA ameniambia hivi, Mimi nitatulia, na kuangalia katika makazi yangu, kama wakati wa mwangaza mweupe wa jua kali, mfano wa wingu la umande katika hari ya mavuno. Maana kabla ya mavuno, maua yaangukapo, na maua yakawa zabibu zianzazo kuiva, ndipo atakapoyakata matawi kwa miundu, na kuviondoa vitawi vilivyopanuka na kuvikata.
Isaya 18:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ole kwa nchi ya mvumo wa mabawa, kando ya mito ya Kushi, iwapelekayo wajumbe wake kupitia bahari kwa mashua za mafunjo juu ya maji. Nendeni, wajumbe wepesi, kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo, kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu, taifa gomvi lenye lugha ngeni, ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito. Enyi mataifa yote ya ulimwengu, ninyi mnaoishi duniani wakati bendera itakapoinuliwa milimani, mtaiona, nayo tarumbeta itakapolia, mtaisikia. Hili ndilo BWANA aliloniambia: “Nitatulia kimya na kutazama kutoka maskani yangu, kama joto linalometameta katika mwanga wa jua, kama wingu la umande katika joto la wakati wa mavuno.” Kwa maana, kabla ya mavuno, wakati wa kuchanua ukishapita na maua yakawa zabibu zinazoiva, atayakata machipukizi kwa mundu wa kupogolea matawi, naye atakata na kuyaondoa matawi yaliyopanuka.