Isaya 14:9-16
Isaya 14:9-16 Biblia Habari Njema (BHN)
“Kuzimu nako kumechangamka, ili kukulaki wakati utakapokuja. Kunaiamsha mizimu ije kukusalimu na wote waliokuwa wakuu wa dunia; huwaamsha kutoka viti vyao vya enzi wote waliokuwa wafalme wa mataifa. Wote kwa pamoja watakuambia: ‘Nawe pia umedhoofika kama sisi! Umekuwa kama sisi wenyewe! Fahari yako imeteremshwa kuzimu pamoja na muziki wa vinubi vyako. Chini mabuu ndio kitanda chako, na wadudu ndio blanketi lako!’ “Jinsi gani ulivyoporomoshwa toka mbinguni, wewe uliyekuwa nyota angavu ya alfajiri. Jinsi gani ulivyoangushwa chini, wewe uliyeyashinda mataifa! Wewe ulijisemea moyoni mwako: ‘Nitapanda mpaka mbinguni; nitaweka kiti changu juu ya nyota za Mungu, nitaketi juu ya mlima wakutanapo miungu, huko mbali pande za kaskazini. Nitapanda vilele vya mawingu nitajifanya kuwa sawa na Mungu Mkuu.’ Lakini umeporomoshwa hadi kuzimu; umeshushwa chini kabisa shimoni. “Watakaokuona watakukodolea macho, watakushangaa wakisema: ‘Je, huyu ndiye aliyetetemesha dunia na kuzitikisa falme
Isaya 14:9-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao vya enzi. Hao wote watajibu na kukuambia, Je! Wewe nawe umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe umekuwa kama sisi! Fahari yako imeshushwa hadi kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika. Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye Juu. Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo. Wao wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme
Isaya 14:9-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao vya enzi. Hao wote watajibu na kukuambia, Je! Wewe nawe umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe umekuwa kama sisi! Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika. Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo. Wao wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme
Isaya 14:9-16 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kuzimu kumetaharuki kukulaki unapokuja, kunaamsha roho za waliokufa ili kukupokea, wote waliokuwa viongozi katika ulimwengu, kunawafanya wainuke kwenye viti vyao vya kifalme: wale wote waliokuwa wafalme juu ya mataifa. Wote wataitikia, watakuambia, “Wewe pia umekuwa dhaifu, kama sisi tulivyo; wewe umekuwa kama sisi.” Majivuno yako yote yameshushwa hadi Kuzimu, pamoja na kelele ya vinubi vyako, mafunza yametanda chini yako, na minyoo imekufunika. Tazama jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, ewe nyota ya asubuhi, mwana wa mapambazuko! Umetupwa chini duniani, wewe uliyepata kuangusha mataifa! Ulisema moyoni mwako, “Nitapanda juu hadi mbinguni, nitakiinua kiti changu cha utawala juu ya nyota za Mungu; nitaketi nimetawazwa juu ya mlima wa kusanyiko, kwenye vimo vya juu sana vya Mlima Mtakatifu. Nitapaa juu kupita mawingu, nitajifanya kama Yeye Aliye Juu Sana.” Lakini umeshushwa chini hadi Kuzimu, hadi kwenye vina vya shimo. Wale wanaokuona wanakukazia macho, wanatafakari hatima yako: “Je, huyu ndiye yule aliyetikisa dunia na kufanya falme zitetemeke