Isaya 14:13-14
Isaya 14:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Wewe ulijisemea moyoni mwako: ‘Nitapanda mpaka mbinguni; nitaweka kiti changu juu ya nyota za Mungu, nitaketi juu ya mlima wakutanapo miungu, huko mbali pande za kaskazini. Nitapanda vilele vya mawingu nitajifanya kuwa sawa na Mungu Mkuu.’
Isaya 14:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye Juu.
Isaya 14:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.
Isaya 14:13-14 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ulisema moyoni mwako, “Nitapanda juu hadi mbinguni, nitakiinua kiti changu cha utawala juu ya nyota za Mungu; nitaketi nimetawazwa juu ya mlima wa kusanyiko, kwenye vimo vya juu sana vya Mlima Mtakatifu. Nitapaa juu kupita mawingu, nitajifanya kama Yeye Aliye Juu Sana.”