Isaya 13:9-13
Isaya 13:9-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Siku ya Mwenyezi-Mungu inakuja, siku kali, ya ghadhabu na hasira kali. Itaifanya nchi kuwa uharibifu, itawaangamiza wenye dhambi wake. Nyota na vilimia vyake angani hazitaangaza; jua linapochomoza litakuwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake. Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nitauadhibu ulimwengu kwa uovu wake, waovu kwa sababu ya makosa yao. Nitakikomesha kiburi cha wenye majivuno, na kuporomosha ubaradhuli wa watu katili. Nitawafanya watu kuwa wachache kuliko dhahabu safi; binadamu watakuwa wachache kuliko dhahabu ya Ofiri. Nitazitetemesha mbingu nayo nchi itatikisika katika misingi yake kwa sababu ya ghadhabu yangu Mwenyezi-Mungu siku ile ya hasira yangu kali.
Isaya 13:9-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tazama, siku ya BWANA inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake. Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze. Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayashusha chini majivuno yao walio wakali; nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri. Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake, kwa sababu ya ghadhabu ya BWANA wa majeshi, na kwa sababu ya siku ya hasira yake kali.
Isaya 13:9-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tazama, siku ya BWANA inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake. Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze. Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali; nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri. Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake, kwa sababu ya ghadhabu ya BWANA wa majeshi, na kwa sababu ya siku ya hasira yake kali.
Isaya 13:9-13 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Tazameni, siku ya BWANA inakuja, siku katili, yenye ghadhabu na hasira kali, kuifanya nchi kuwa ukiwa, na kuwaangamiza wenye dhambi waliomo. Nyota za mbinguni na makundi ya nyota havitatoa mwanga wake. Jua linalochomoza litatiwa giza na mwezi hautatoa nuru yake. Nitauadhibu ulimwengu kwa ajili ya uovu wake, waovu kwa ajili ya dhambi zao. Nitakomesha majivuno ya wenye kiburi, na nitakishusha kiburi cha watu wakatili. Nitawafanya wanadamu kuwa adimu kuliko dhahabu safi, watakuwa wachache sana kuliko dhahabu ya Ofiri. Kwa hiyo nitazifanya mbingu zitetemeke, nayo dunia itatikisika kutoka mahali pake katika ghadhabu ya BWANA wa majeshi, katika siku ya hasira yake iwakayo.