Isaya 13:6-9
Isaya 13:6-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Lieni maana siku ya Mwenyezi-Mungu imekaribia; inakuja kama maafa kutoka kwa Mungu Mwenye Nguvu. Kwa hiyo mikono ya kila mtu italegea, kila mtu atakufa moyo. Watu watafadhaika, watashikwa na hofu na maumivu, watakuwa na uchungu kama mama anayejifungua. Watatazamana kwa mashaka, nyuso zao zitawaiva kwa haya. Siku ya Mwenyezi-Mungu inakuja, siku kali, ya ghadhabu na hasira kali. Itaifanya nchi kuwa uharibifu, itawaangamiza wenye dhambi wake.
Isaya 13:6-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Pigeni kelele za hofu; maana siku ya BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu hiyo mikono yote italegea, na moyo wa kila mtu utayeyuka. Nao watafadhaika; watashikwa na uchungu na maumivu; watakuwa na uchungu kama mwanamke aliye karibu kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto. Tazama, siku ya BWANA inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
Isaya 13:6-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Pigeni kelele za hofu; maana siku ya BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu hiyo mikono yote italegea, na moyo wa kila mtu utayeyuka. Nao watafadhaika; watashikwa na utungu na maumivu; watakuwa na utungu kama mwanamke aliye karibu na kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto. Tazama, siku ya BWANA inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
Isaya 13:6-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ombolezeni, kwa maana siku ya BWANA i karibu, itakuja kama uharibifu kutoka kwa Mwenyezi. Kwa sababu ya hili, mikono yote italegea, moyo wa kila mtu utayeyuka. Hofu itawakamata, uchungu na maumivu makali yatawashika, watagaagaa kama mwanamke aliye na uchungu wa kuzaa. Watatazamana kwa hofu kila mtu na mwenzake, nyuso zao zikiwaka kama moto. Tazameni, siku ya BWANA inakuja, siku katili, yenye ghadhabu na hasira kali, kuifanya nchi kuwa ukiwa, na kuwaangamiza wenye dhambi waliomo.