Isaya 12:2-6
Isaya 12:2-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu ndiye mwenye kuniokoa, nitamtegemea yeye, wala sitaogopa; Mwenyezi-Mungu hunijalia nguvu; yeye mwenyewe ndiye aniokoaye.” Mtachota maji kwa furaha kutoka visima vya wokovu. Siku hiyo mtasema: “Mshukuruni Mwenyezi-Mungu mwombeni kwa jina lake. Yajulisheni mataifa matendo yake, tangazeni kuwa jina lake limetukuka. Mwimbieni Mwenyezi-Mungu sifa kwa kuwa ametenda mambo makuu; haya na yajulikane duniani kote. Pazeni sauti na kuimba kwa furaha, enyi wakazi wa Siyoni, maana aliye mkuu miongoni mwenu ndiye Mungu, Mtakatifu wa Israeli.”
Isaya 12:2-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu. Na katika siku hiyo mtasema, Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake; Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa, Litangazeni jina lake kuwa limetukuka. Mwimbieni BWANA; kwa kuwa ametenda makuu; Na yajulikane haya katika dunia yote. Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
Isaya 12:2-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu. Na katika siku hiyo mtasema, Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake; Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa, Litajeni jina lake kuwa limetukuka. Mwimbieni BWANA; kwa kuwa ametenda makuu; Na yajulikane haya katika dunia yote. Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
Isaya 12:2-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hakika Mungu ni wokovu wangu; nitamtumaini wala sitaogopa. BWANA, BWANA, ni nguvu zangu na wimbo wangu; amekuwa wokovu wangu.” Kwa furaha mtachota maji kutoka visima vya wokovu. Katika siku hiyo mtasema: “Mshukuruni BWANA, mliitie jina lake; julisheni miongoni mwa mataifa yale aliyoyafanya, tangazeni kuwa jina lake limetukuka. Mwimbieni BWANA, kwa kuwa ametenda mambo makuu, hili na lijulikane duniani kote. Pazeni sauti mwimbe kwa furaha, watu wa Sayuni, kwa maana mkuu ni yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli miongoni mwenu.”