Hosea 5:5-15
Hosea 5:5-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Kiburi cha Waisraeli chaonekana wazi; watu wa Efraimu watajikwaa katika hatia yao, nao watu wa Yuda watajikwaa pamoja nao. Watakwenda na makundi yao ya kondoo na ng'ombe, kumtafuta Mwenyezi-Mungu; lakini hawataweza kumpata, kwa sababu amejitenga nao. Wamevunja uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, wamezaa watoto walio haramu. Mwezi mwandamo utawaangamiza, pamoja na mashamba yao. “Pigeni baragumu huko Gibea, na tarumbeta huko Rama. Pigeni king'ora huko Beth-aveni. Enyi watu wa Benyamini, adui yenu yuko nyuma! Siku nitakapotoa adhabu Efraimu itakuwa kama jangwa! Ninachotangaza miongoni mwa makabila ya Israeli, ni jambo litakalotukia kwa hakika. Viongozi wa Yuda wamekuwa wenye kubadili mipaka ya ardhi. Mimi nitawamwagia hasira yangu kama maji. Efraimu ameteswa, haki zake zimetwaliwa; kwani alipania kufuata upuuzi. Hivyo mimi Mungu niko kama nondo kwa Efraimu, kama donda baya kwa watu wa Yuda. Watu wa Efraimu walipogundua ugonjwa wao, naam, watu wa Yuda walipogundua donda lao, watu wa Efraimu walikwenda Ashuru kuomba msaada kwa mfalme mkuu; lakini yeye hakuweza kuwatibu, hakuweza kuponya donda lenu. Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu, kama mwanasimba kwa watu wa Yuda. Mimi mwenyewe nitawararua na kuondoka, nitawachukua na hakuna atakayewaokoa. Nitarudi mahali pangu na kujitenga nao mpaka wakiri kosa lao na kunirudia. Taabu zao zitawafundisha wanitafute, wakisema
Hosea 5:5-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; kwa sababu hiyo, Israeli na Efraimu watajikwaa katika uovu wao. Yuda naye atajikwaa pamoja nao. Watakwenda na makundi yao ya kondoo na ng'ombe wamtafute BWANA; lakini hawatamwona; amejitenga nao. Wamemtendea BWANA kwa hila; maana wamezaa wana wageni; sasa mwezi huu uandamao utawaangamiza pamoja na mashamba yao. Pigeni tarumbeta katika Gibea, na baragumu katika Rama; pazeni sauti ya hofu katika Beth-aveni; nyuma yako, Ee Benyamini! Efraimu atakuwa ukiwa siku ya adhabu; katika makabila ya Israeli nimetangaza jambo litakalotukia kweli. Wakuu wa Yuda ni kama watu waondoao alama ya mpaka; nitawamwagia ghadhabu yangu kama maji. Efraimu ameonewa, amesetwa katika hukumu, kwa sababu alikuwa radhi kufuata ubatili. Kwa sababu hiyo mimi nimekuwa kama nondo kwa Efraimu, nimekuwa kama ubovu kwa nyumba ya Yuda. Efraimu alipouona ugonjwa wake, na Yuda jeraha lake, ndipo Efraimu alipokwenda kwa Ashuru, akatuma watu kwa mfalme Yarebu; lakini yeye hawezi kuwapoza, wala hatawaponya jeraha lenu. Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu, na kama mwanasimba kwa nyumba ya Yuda; mimi, naam, mimi nitararua, kisha nitakwenda zangu; nitachukua mbali, wala hapatakuwa na mtu wa kuokoa. Nitakwenda zangu niparudie mahali pangu, hata watakapoungama makosa yao na kunitafuta uso wangu; katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.
Hosea 5:5-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; kwa sababu hiyo, Israeli na Efraimu watajikwaa katika uovu wao. Yuda naye atajikwaa pamoja nao. Watakwenda na makundi yao ya kondoo na ng’ombe wamtafute BWANA; lakini hawatamwona; amejitenga nao. Wametenda kwa hila juu ya BWANA; maana wamezaa wana wageni; sasa mwezi huu uandamao utawala pamoja na mashamba yao. Pigeni tarumbeta katika Gibea, na baragumu katika Rama; pazeni sauti ya hofu katika Beth-Aveni; nyuma yako, Ee Benyamini! Efraimu atakuwa ukiwa siku ya kukemewa; katika kabila za Israeli nimetangaza habari itakayotokea halafu bila shaka. Wakuu wa Yuda ni kama watu waondoao alama ya mpaka; nitawamwagia ghadhabu yangu kama maji. Efraimu ameonewa, amesetwa katika hukumu, kwa sababu alikuwa radhi kufuata ubatili. Kwa sababu hiyo mimi nimekuwa kama nondo kwa Efraimu, nimekuwa kama ubovu kwa nyumba ya Yuda. Efraimu alipouona ugonjwa wake, na Yuda jeraha yake, ndipo Efraimu alipokwenda kwa Ashuru, akatuma watu kwa mfalme Yarebu; lakini yeye hawezi kuwapoza, wala hatawaponya jeraha yenu. Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu, na kama mwana-simba kwa nyumba ya Yuda; mimi, naam, mimi nitararua, kisha nitakwenda zangu; nitachukulia mbali, wala hapatakuwa na mtu wa kupokonya. Nitakwenda zangu niparudie mahali pangu, hata watakapoungama makosa yao na kunitafuta uso wangu; katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.
Hosea 5:5-15 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kiburi cha Israeli kinashuhudia dhidi yao; Waisraeli, hata Efraimu, wanajikwaa katika dhambi zao; pia Yuda atajikwaa pamoja nao. Wanapoenda na makundi yao ya kondoo na ngʼombe kumtafuta BWANA, hawatampata; yeye amejiondoa kutoka kwao. Wao si waaminifu kwa BWANA; wamezaa watoto haramu. Sasa sikukuu zao za Mwandamo wa Mwezi zitawaangamiza wao pamoja na mashamba yao. “Pigeni tarumbeta huko Gibea, na baragumu huko Rama. Pazeni kelele za vita huko Beth-Aveni; ongoza, ee Benyamini. Efraimu ataachwa ukiwa katika siku ya kuadhibiwa. Miongoni mwa makabila ya Israeli ninatangaza lile ambalo halina budi kutukia. Viongozi wa Yuda ni kama wale wanaosogeza mawe ya mpaka. Nitamwaga ghadhabu yangu juu yao kama mafuriko ya maji. Efraimu amedhulumiwa, amekanyagwa katika hukumu kwa kuwa amekusudia kufuatia sanamu. Mimi ni kama nondo kwa Efraimu, na kama uozo kwa watu wa Yuda. “Efraimu alipoona ugonjwa wake, naye Yuda vidonda vyake, ndipo Efraimu aligeukia Ashuru, na kuomba msaada kwa mfalme mkuu. Lakini hawezi kukuponya, hawezi kukuponya vidonda vyako. Kwa maana nitakuwa kama simba kwa Efraimu, kama simba mkubwa kwa Yuda. Nitawararua vipande vipande na kuondoka; nitawachukua mbali, na hakuna wa kuwaokoa. Kisha nitarudi mahali pangu hadi watakapokubali kosa lao. Nao watautafuta uso wangu; katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.”