Hosea 5:1-4
Hosea 5:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
“Haya! Sikilizeni enyi makuhani! Tegeni sikio, enyi Waisraeli! Sikilizeni enyi ukoo wa kifalme! Nyinyi mlipaswa kuzingatia haki, badala yake mmekuwa mtego huko Mizpa, mmekuwa wavu wa kuwanasa huko Tabori. Mmechimba shimo refu la kuwanasa huko Shitimu. Lakini mimi nitawaadhibuni nyote. Nawajua watu wa Efraimu, Waisraeli hawakufichika kwangu. Nyinyi watu wa Efraimu mmefanya uzinzi, watu wote wa Israeli wamejitia najisi. “Matendo yao yanawazuia wasimrudie Mungu wao. Mioyoni mwao wamejaa uzinzi; hawanijui mimi Mwenyezi-Mungu.
Hosea 5:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sikieni haya, enyi makuhani, sikilizeni, enyi nyumba ya Israeli, tegeni masikio yenu, enyi wa nyumba ya mfalme, kwa kuwa hukumu hii yawahusu ninyi; maana mmekuwa mtego huko Mizpa, na wavu uliotandwa juu ya Tabori. Nao walioasi wameongeza sana ufisadi wao; lakini mimi ndiye awakaripiaye wote pia. Mimi namjua Efraimu, wala Israeli hakufichwa nisimwone; maana sasa, Ee Efraimu, umefanya uzinzi; Israeli ametiwa unajisi. Matendo yao hayatawaacha kumgeukia Mungu wao; maana roho ya uzinzi imo ndani yao, wala hawamjui BWANA.
Hosea 5:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Sikieni haya, enyi makuhani, sikilizeni, enyi nyumba ya Israeli, tegeni masikio yenu, enyi wa nyumba ya mfalme, kwa kuwa hukumu hii yawahusu ninyi; maana mmekuwa mtego huko Mizpa, na wavu uliotandwa juu ya Tabori. Nao walioasi wameongeza sana ufisadi wao; lakini mimi ndiye awakaripiaye wote pia. Mimi namjua Efraimu, wala Israeli hakufichwa nisimwone; maana sasa, Ee Efraimu, umefanya uzinzi; Israeli ametiwa unajisi. Matendo yao hayatawaacha kumgeukia Mungu wao; maana roho ya uzinzi imo ndani yao, wala hawamjui BWANA.
Hosea 5:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Sikieni hili, enyi makuhani! Kuweni wasikivu, enyi Waisraeli! Sikieni, ee nyumba ya mfalme! Hukumu hii ni dhidi yenu: Mmekuwa mtego huko Mispa, wavu uliotandwa juu ya Tabori. Waasi wamezidisha sana mauaji. Mimi nitawatiisha wote. Ninajua yote kuhusu Efraimu, Israeli hukufichika kwangu. Efraimu, sasa umegeukia ukahaba, Israeli amenajisika. “Matendo yao hayawaachii kurudi kwa Mungu wao. Roho ya ukahaba iko ndani ya mioyo yao, hawamkubali BWANA.