Hosea 4:1-5
Hosea 4:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Msikilizeni Mwenyezi-Mungu, enyi Waisraeli. Mwenyezi-Mungu anawashutumu wakazi wa nchi hii. “Hamna tena uaminifu wala wema nchini; hamna anayemjua Mungu katika nchi hii. Kuapa, uongo, mauaji, wizi na uzinzi huzuka humo. Umwagaji damu hufuatana mfululizo. Kwa hiyo, nchi yote ni kame, wakazi wake wote wanaangamia pamoja na wanyama wa porini na ndege; hata samaki wa baharini wanaangamizwa. “Lakini watu wasilaumiwe, wasishutumiwe; maana mimi nakushutumu wewe kuhani. Wewe utajikwaa mchana, naye nabii atajikwaa pamoja nawe usiku. Nitamwangamiza mama yako Israeli.
Hosea 4:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lisikieni neno la BWANA, enyi wana wa Israeli; kwa maana BWANA ana shutuma nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi. Hapana neno ila kuapa kwa uongo, na kuvunja ahadi, na kuua, na kuiba, na kuzini; huruka mpaka, na kumwaga damu mfululizo. Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na kila mtu akaaye ndani yake atadhoofika, pamoja na wanyama wa porini na ndege wa angani; naam, samaki wa baharini pia wataangamizwa. Lakini asishindane mtu, wala mtu asikemee; maana watu wako ni kama wao washindanao na kuhani. Na wewe utajikwaa wakati wa mchana, na nabii naye atajikwaa pamoja nawe wakati wa usiku; nami nitamwangamiza mama yako.
Hosea 4:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lisikieni neno la BWANA, enyi wana wa Israeli; kwa maana BWANA ana mateto nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi. Hapana neno ila kuapa kwa uongo, na kuvunja ahadi, na kuua, na kuiba, na kuzini; huruka mpaka, na damu hugusana na damu. Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na kila mtu akaaye ndani yake atadhoofika, pamoja na wanyama wa kondeni na ndege wa angani; naam, samaki wa baharini pia wataondolewa. Walakini asishindane mtu, wala mtu asikemee; maana watu wako ni kama wao washindanao na kuhani. Na wewe utajikwaa wakati wa mchana, na nabii naye atajikwaa pamoja nawe wakati wa usiku; nami nitamwangamiza mama yako.
Hosea 4:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Sikieni neno la BWANA, enyi Waisraeli, kwa sababu BWANA analo shtaka dhidi yenu ninyi mnaoishi katika nchi: “Hakuna uaminifu, hakuna upendo, hakuna kumjua Mungu katika nchi. Kuna kulaani tu, uongo na uuaji, wizi na uzinzi, bila kuwa na mipaka, nao umwagaji damu mmoja baada ya mwingine. Kwa sababu hii nchi huomboleza, wote wanaoishi ndani yake wanadhoofika; wanyama wa kondeni, ndege wa angani na samaki wa baharini wanakufa. “Lakini mtu yeyote na asilete shtaka, mtu yeyote na asimlaumu mwenzake, kwa maana watu wako ni kama wale waletao mashtaka dhidi ya kuhani. Unajikwaa usiku na mchana, nao manabii hujikwaa pamoja nawe. Kwa hiyo nitamwangamiza mama yako