Hosea 12:3-5
Hosea 12:3-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu ana mashtaka dhidi ya Yuda; atawaadhibu wazawa wa Yakobo kadiri ya makosa yao, na kuwalipa kadiri ya matendo yao. Yakobo akiwa bado tumboni mwa mama yake, alimshika kisigino kaka yake. Na alipokuwa mtu mzima alishindana na Mungu. Alipambana na malaika, akamshinda; alilia machozi na kuomba ahurumiwe. Huko Betheli, alikutana na Mungu, huko Mungu aliongea naye.
Hosea 12:3-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tumboni alimshika ndugu yake kisigino; Na alipokuwa mtu mzima alishindana na Mungu; Naam, alishindana na malaika Akashinda; alilia, na kumsihi; Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko; Naam, BWANA, Mungu wa majeshi; BWANA ndilo kumbukumbu lake.
Hosea 12:3-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tumboni alimshika ndugu yake kisigino; Na alipokuwa mtu mzima alikuwa na uwezo kwa Mungu; Naam, alikuwa na uwezo juu ya malaika Akashinda; alilia, na kumsihi; Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko; Naam, BWANA, Mungu wa majeshi; BWANA ndilo kumbukumbu lake.
Hosea 12:3-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Yakobo akiwa tumboni alishika kisigino cha kaka yake; kama mwanadamu, alishindana na Mungu. Alishindana na malaika na kumshinda; alilia na kuomba upendeleo wake. Alimkuta huko Betheli na kuzungumza naye huko: BWANA Mungu wa majeshi, BWANA ndilo jina lake!