Hosea 12:2-4
Hosea 12:2-4 Biblia Habari Njema (BHN)
“Watu wa Efraimu wanachunga upepo kutwa nzima wanafukuza upepo wa mashariki. Wanazidisha uongo na ukatili, wanafanya mkataba na Ashuru na kupeleka mafuta Misri.” Mwenyezi-Mungu ana mashtaka dhidi ya Yuda; atawaadhibu wazawa wa Yakobo kadiri ya makosa yao, na kuwalipa kadiri ya matendo yao. Yakobo akiwa bado tumboni mwa mama yake, alimshika kisigino kaka yake. Na alipokuwa mtu mzima alishindana na Mungu.
Hosea 12:2-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA naye ana shutuma juu ya Yuda, naye atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake; kwa kadiri ya matendo yake atamlipa. Tumboni alimshika ndugu yake kisigino; Na alipokuwa mtu mzima alishindana na Mungu; Naam, alishindana na malaika Akashinda; alilia, na kumsihi; Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko
Hosea 12:2-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA naye ana mateto na Yuda, naye atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake; kwa kadiri ya matendo yake atamlipa. Tumboni alimshika ndugu yake kisigino; Na alipokuwa mtu mzima alikuwa na uwezo kwa Mungu; Naam, alikuwa na uwezo juu ya malaika Akashinda; alilia, na kumsihi; Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko
Hosea 12:2-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA analo shtaka dhidi ya Yuda, atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake na kumlipa kwa kadiri ya matendo yake. Yakobo akiwa tumboni alishika kisigino cha kaka yake; kama mwanadamu, alishindana na Mungu. Alishindana na malaika na kumshinda; alilia na kuomba upendeleo wake. Alimkuta huko Betheli na kuzungumza naye huko