Hosea 11:1-3
Hosea 11:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
“Israeli alipokuwa mtoto, nilimpenda, Kutoka Misri nilimwita mwanangu. Lakini kadiri nilivyozidi kuwaita, ndivyo walivyozidi kwenda mbali nami; waliendelea kuyatambikia Mabaali, na kuvifukizia ubani vinyago vya miungu. Mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea! Mimi mwenyewe niliwachukua mikononi mwangu; lakini hawakutambua kuwa mimi ndiye niliyewatunza.
Hosea 11:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Israeli alipokuwa mtoto, nilikuwa nikimpenda, nikamwita mwanangu atoke Misri. Kadiri walivyowaita ndivyo walivyoondoka na kuwaacha; waliwatolea dhabihu Mabaali, na kuzifukizia uvumba sanamu za kuchonga. Lakini nilimfundisha Efraimu kwenda kwa miguu; niliwachukua mikononi mwangu; hawakujua ya kuwa niliwaponya.
Hosea 11:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Israeli alipokuwa mtoto, nalikuwa nikimpenda, nikamwita mwanangu atoke Misri. Kadiri walivyowaita ndivyo walivyoondoka na kuwaacha; waliwatolea dhabihu Mabaali, na kuzifukizia uvumba sanamu za kuchonga. Lakini nalimfundisha Efraimu kwenda kwa miguu; naliwachukua mikononi mwangu; hawakujua ya kuwa naliwaponya.
Hosea 11:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Israeli alipokuwa mtoto, nilimpenda; nilimwita mwanangu kutoka Misri. Lakini kadiri nilivyomwita Israeli, ndivyo walivyoenda mbali nami. Walitoa dhabihu kwa Mabaali na kufukiza uvumba kwa vinyago. Mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea, nikiwashika mikono; lakini hawakutambua kuwa ni mimi niliyewaponya.