Hosea 10:11-13
Hosea 10:11-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Efraimu ni ndama aliyefundishwa vizuri, akapenda kupura nafaka. Lakini sasa shingo yake nzuri nitaifunga nira. Yuda atalima kwa jembe yeye mwenyewe, naam, Yakobo atakokota jembe la kupalilia. Pandeni wema kwa faida yenu, nanyi mtavuna upendo; limeni mashamba yaliyoachwa, maana wakati wa kunitafuta mimi Bwana umefika nami nitawanyeshea baraka. Lakini nyinyi mmepanda uovu, nyinyi mmevuna dhuluma; mmekula matunda ya uongo wenu. Wewe Israeli ulitegemea nguvu zako mwenyewe, na wingi wa askari wako.
Hosea 10:11-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Naye Efraimu ni ndama aliyefundishwa, apendaye kupura; lakini nimepitisha kongwa juu ya shingo yake nzuri; nitampandisha mwenye kupanda juu ya Efraimu; Yuda atalima, na Yakobo atapiga haro yeye mwenyewe. Jipandieni katika haki, vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta BWANA, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki. Mmelima dhuluma, mmevuna uovu; mmekula matunda ya uongo; kwa maana uliitumainia njia yako, na wingi wa mashujaa wako.
Hosea 10:11-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Naye Efraimu ni ndama aliyefundishwa, apendaye kupura; lakini nimepitisha kongwa juu ya shingo yake nzuri; nitampandisha mwenye kupanda juu ya Efraimu; Yuda atalima, na Yakobo atavunja madongoa yake. Jipandieni katika haki, vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta BWANA, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki. Mmelima dhuluma, mmevuna uovu; mmekula matunda ya uongo; kwa maana uliitumainia njia yako, na wingi wa mashujaa wako.
Hosea 10:11-13 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Efraimu ni ndama jike aliyefundishwa ambaye hupenda kupura; hivyo nitamfunga nira juu ya shingo yake nzuri. Nitamwendesha Efraimu, Yuda lazima alime, naye Yakobo lazima avunjavunje mabonge ya udongo. Jipandieni wenyewe haki, vuneni matunda ya upendo usio na kikomo, vunjeni ardhi yenu isiyolimwa; kwa kuwa ni wakati wa kumtafuta BWANA, hadi atakapokuja na kuwanyeshea juu yenu haki. Lakini mmepanda uovu, mkavuna ubaya, mmekula tunda la udanganyifu. Kwa sababu mmetegemea nguvu zenu wenyewe na wingi wa mashujaa wenu