Waebrania 6:13-15
Waebrania 6:13-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa jina lake mwenyewe, maana hakuna aliye mkuu kuliko Mungu ambaye kwa huyo angeweza kuapa. Mungu alisema: “Hakika nitakubariki na nitakupa wazawa wengi.” Abrahamu alisubiri kwa uvumilivu na hivyo akapokea kile alichoahidiwa na Mungu.
Waebrania 6:13-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa maana Mungu, alipompa Abrahamu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake, akisema, Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza. Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi.
Waebrania 6:13-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa maana Mungu, alipompa Ibrahimu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake, akisema, Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza. Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi.
Waebrania 6:13-15 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mungu alipompa Abrahamu ahadi yake, kwa sababu hapakuwa mwingine mkuu kuliko yeye ambaye angeapa naye, aliapa kwa nafsi yake, akisema, “Hakika nitakubariki na kukupa wazao wengi.” Abrahamu naye, baada ya kungoja kwa saburi, alipokea kile kilichoahidiwa.