Hagai 1:5-7
Hagai 1:5-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Sasa hili ndilo asemalo BWANA wa majeshi: “Zitafakarini vyema njia zenu. Mmepanda vingi, lakini mmevuna haba. Mnakula lakini hamshibi, mnakunywa, lakini hamtosheki. Mnavaa nguo, lakini hamsikii joto. Mnapata mishahara, lakini inatoweka kama imewekwa kwenye mfuko uliotobokatoboka.” Hili ndilo asemalo BWANA wa majeshi: “Zitafakarini vyema njia zenu.
Hagai 1:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Sasa, asema hivi Mwenyezi-Mungu: “Fikirini kama mnafanya sawa! Nyinyi mmepanda mbegu kwa wingi, lakini mmevuna kidogo; mnakula, lakini hamshibi; mnakunywa divai, lakini hamtosheki; mnavaa nguo, lakini bado mnasikia baridi; mfanyakazi mshahara wake huwa kama umetumbukizwa katika mfuko uliotoboka.” Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Fikirini kama mnafanya sawa!
Hagai 1:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi sasa, BWANA wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu. Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamtosheki na vinywaji; mnajivika nguo lakini hampati joto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotobokatoboka. BWANA wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.
Hagai 1:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi sasa, BWANA wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu. Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka. BWANA wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.