Hagai 1:2-4
Hagai 1:2-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Hagai akasema: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: Watu hawa wanasema kwamba wakati wa kulijenga upya hekalu langu haujafika.” Lakini Mwenyezi-Mungu ameniambia mimi nabii Hagai, “Je, ni sawa kwenu kukaa katika majumba yenu ya fahari hali hekalu langu ni magofu matupu?”
Hagai 1:2-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Watu hawa husema, Wakati wa kuijenga upya nyumba ya BWANA haujafika. Ndipo neno la BWANA lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema, Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika?
Hagai 1:2-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Watu hawa husema, Huu sio wakati utupasao kuja, huu sio wakati wa kujenga nyumba ya BWANA. Ndipo neno la BWANA lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema, Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika?
Hagai 1:2-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hivi ndivyo asemavyo BWANA wa majeshi: “Hawa watu husema, ‘Wakati haujawadia wa kujenga nyumba ya BWANA.’ ” Kisha neno la BWANA likaja kupitia kwa nabii Hagai: “Je, ni wakati wenu ninyi wa kuishi katika nyumba zenu zilizojengwa vizuri, wakati hii nyumba ikibaki gofu?”