Hagai 1:12-15
Hagai 1:12-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Ndipo Zerubabeli mwana wa Shealtieli, na kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki, pamoja na watu wote waliokuwa wamerudi kutoka uhamishoni wakafanya kama Mwenyezi-Mungu, Mungu wao alivyowaambia na kama walivyoambiwa na nabii Hagai, kama alivyotumwa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Watu wakamcha Mwenyezi-Mungu. Kisha Hagai, mjumbe wa Mwenyezi-Mungu, akawapa watu ujumbe ufuatao kutoka kwa Mwenyezi-Mungu: Mwenyezi-Mungu asema: “Mimi nipo pamoja nanyi.” Basi, Mwenyezi-Mungu akawapa moyo Zerubabeli mkuu wa Yuda, kuhani mkuu Yoshua na watu wote waliokuwa wamerudi kutoka uhamishoni, walishughulikie hekalu. Walianza kazi hiyo ya kulijenga upya hekalu la Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wao, mnamo siku ya ishirini na nne ya mwezi wa sita, mwaka wa pili wa utawala wa mfalme Dario.
Hagai 1:12-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, pamoja na hao watu wote waliokuwa wamebaki, wakaitii sauti ya BWANA, Mungu wao, na maneno ya nabii Hagai, kama BWANA, Mungu wao, alivyomtuma; nao watu wakaogopa mbele za BWANA. Ndipo Hagai mjumbe wa BWANA, katika ujumbe wa BWANA, akawaambia watu ujumbe wa BWANA, akisema, Mimi nipo pamoja nanyi, asema BWANA. BWANA akaiamsha roho ya Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na roho ya Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na roho za watu waliokuwa wamebaki; wakaenda, wakafanya kazi katika nyumba ya BWANA wa majeshi, Mungu wao; katika siku ya ishirini na nne ya mwezi, katika mwezi wa sita, katika mwaka wa pili wa mfalme Dario.
Hagai 1:12-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, pamoja na hayo mabaki yote ya watu, wakaitii sauti ya BWANA, Mungu wao, na maneno ya Hagai nabii, kama BWANA, Mungu wao, alivyomtuma; nao watu wakaogopa mbele za BWANA. Ndipo Hagai mjumbe wa BWANA, katika ujumbe wa BWANA, akawaambia watu, akisema, Mimi nipo pamoja nanyi, asema BWANA. BWANA akaiamsha roho ya Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda, na roho ya Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na roho zao mabaki ya watu; wakaenda, wakafanya kazi katika nyumba ya BWANA wa majeshi, Mungu wao; katika siku ya ishirini na nne ya mwezi, katika mwezi wa sita, katika mwaka wa pili wa Dario mfalme.
Hagai 1:12-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kisha Zerubabeli mwana wa Shealtieli, Yoshua kuhani mkuu mwana wa Yehosadaki, pamoja na mabaki yote ya watu wakaitii sauti ya BWANA Mungu wao pamoja na ujumbe wa nabii Hagai, kwa sababu alikuwa ametumwa na BWANA Mungu wao. Watu walimwogopa BWANA. Kisha Hagai, mjumbe wa BWANA, akawapa watu ujumbe huu wa BWANA: “Mimi niko pamoja nanyi,” asema BWANA. Kwa hiyo BWANA akachochea roho ya Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na roho ya kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki, pamoja na roho za mabaki yote ya watu. Walikuja wakaanza kufanya kazi katika nyumba ya BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wao, katika siku ya ishirini na nne mwezi wa sita, katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario.