Habakuki 2:15-16
Habakuki 2:15-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Ole wako unayewalewesha jirani zako, na kutia sumu katika divai yao ili upate kuwaona wamekaa uchi. Utajaa aibu badala ya heshima. Utakunywa wewe mwenyewe na kupepesuka! Mwenyezi-Mungu mwenyewe atakulevya, na aibu itaifunika heshima yako!
Habakuki 2:15-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao! Umejaa aibu badala ya utukufu; unywe nawe, uwe kama mtu asiyetahiriwa; kikombe cha mkono wa kulia wa BWANA kitageuzwa ukipokee, na aibu kuu itakuwa juu ya utukufu wako.
Habakuki 2:15-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao! Umejaa aibu badala ya utukufu; unywe nawe, uwe kama mtu asiyetahiriwa; kikombe cha mkono wa kuume wa BWANA kitageuzwa ukipokee, na aibu kuu itakuwa juu ya utukufu wako.
Habakuki 2:15-16 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Ole wake yeye awapaye majirani zake kileo, akikimimina kutoka kwa kiriba cha mvinyo hadi wamelewa, ili apate kutazama miili yao iliyo uchi. Utajazwa na aibu badala ya utukufu. Sasa ni zamu yako! Kunywa na ujifunue! Kikombe kutoka mkono wa kuume wa BWANA kinakujia, na aibu itafunika utukufu wako.