Habakuki 2:1-2
Habakuki 2:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Mimi nitasimama mahali pa kuchungulia, na kukaa juu mnarani; nitakaa macho nione ataniambia nini, atajibu nini kuhusu lalamiko langu.” Kisha, Mwenyezi-Mungu akanijibu hivi: “Yaandike maono haya; yaandike wazi juu ya vibao, anayepitia hapo apate kuyasoma.
Habakuki 2:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu kuhusu kulalamika kwangu. BWANA akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji.
Habakuki 2:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu. BWANA akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji.
Habakuki 2:1-2 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nitasimama katika zamu yangu, na kujiweka juu ya maboma; nitatazama nione atakaloniambia, na jibu nitakalotoa kuhusu lalamiko hili. BWANA Kisha BWANA akajibu: “Andika ufunuo huu, na ukaufanye wazi juu ya vibao, ili mpiga mbiu akimbie nao.