Habakuki 1:11-13
Habakuki 1:11-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha wanasonga mbele kama upepo, wafanya makosa na kuwa na hatia, maana, nguvu zao ndizo mungu wao!” “Je, wewe si ndiwe Mwenyezi-Mungu, tangu kale na kale? Wewe ndiwe Mungu wangu, Mtakatifu wangu, usiyekufa Ee Mwenyezi-Mungu, umewateua Wakaldayo watuhukumu; Ewe Mwamba, umewaimarisha ili watuadhibu! Wewe ni mtakatifu kabisa, huwezi kutazama uovu, huwezi kustahimili kamwe kuona mabaya. Mbona basi wawaona wafanya maovu na kunyamaza, kwa nini unanyamaza waovu wanapowamaliza wale watu walio waadilifu kuliko wao?
Habakuki 1:11-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha atapita kwa kasi, kama upepo, atapita na kuwa ana hatia; yeye ambaye nguvu zake ni mungu wake. Ee BWANA, Mungu wangu, mtakatifu wangu, wewe si wa milele? Hatutakufa. Ee BWANA, umemwandikia hukumu, nawe, Ee Jabali, umemweka imara ili aadhibishwe. Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye
Habakuki 1:11-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha atapita kwa kasi, kama upepo, atapita na kuwa ana hatia; yeye ambaye nguvu zake ni mungu wake. Ee BWANA, Mungu wangu, mtakatifu wangu, wewe si wa milele? Hatutakufa. Ee BWANA, umemwandikia hukumu, nawe, Ee Jabali, umemweka imara ili aadhibishwe. Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye
Habakuki 1:11-13 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kisha wanapita kasi kama upepo na kusonga mbele: watu wenye hatia, ambao nguvu zao ndio mungu wao.” Ee BWANA, je, wewe sio wa tangu milele? Mungu wangu, Uliye Mtakatifu wangu, hatutakufa. Ee BWANA, umewachagua wao ili watekeleze hukumu; Ee Mwamba, umewaamuru watuadhibu. Macho yako ni safi mno hata yasiweze kuutazama uovu, wala huwezi kuvumilia makosa. Kwa nini basi unawavumilia wadanganyifu? Kwa nini unakuwa kimya wakati waovu wanawameza wale wenye haki kuliko wao wenyewe?