Habakuki 1:1-11
Habakuki 1:1-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ufunuo aliouona nabii Habakuki. Ee BWANA, nilie hata lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa. Mbona wanionyesha uovu, na kunitazamisha ukaidi? Maana uharibifu na udhalimu u mbele yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea. Kwa sababu hiyo sheria imelegea, wala hukumu haipatikani; kwa maana watu wabaya huwazunguka wenye haki; kwa sababu hiyo hukumu ikipatikana imepotoka. Angalieni, enyi mlio kati ya mataifa, katazameni, kastaajabuni sana; kwa maana mimi natenda tendo siku zenu, ambalo hamtaliamini hata mkiambiwa. Kwa maana, angalieni, nawaondokesha Wakaldayo, taifa lile kali, lenye haraka kupita kiasi; wapitao katikati ya dunia, ili wayamiliki makao yasiyo yao. Hao ni watu wa kutisha sana, wa kuogofya sana; hukumu yao na ukuu wao hutoka katika nafsi zao wenyewe. Farasi zao ni wepesi kuliko chui, ni wakali kuliko mbwa-mwitu wa jioni; na wapanda farasi wao hujitapa naam, wapanda farasi wao watoka mbali sana; huruka kama tai afanyaye haraka ale. Waja wote ili kufanya udhalimu; nyuso zao zimeelekezwa kwa bidii yao kama upepo wa mashariki, nao hukusanya mateka kama mchanga. Naam, huwadhihaki wafalme, na wakuu ni kitu cha kudharauliwa kwake; huidharau kila ngome; kwa maana hufanya chungu ya mavumbi, na kuitwaa. Kisha atapita kwa kasi, kama upepo, atapita na kuwa ana hatia; yeye ambaye nguvu zake ni mungu wake.
Habakuki 1:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Kauli ya Mungu aliyoiona nabii Habakuki. “Ee Mwenyezi-Mungu, nitakulilia mpaka lini, nawe usinisikilize na kunisaidia? Kwa nini nalia: ‘Dhuluma’ nawe hutuokoi? Kwa nini wanifanya nishuhudie mabaya na taabu? Uharibifu na ukatili vinanizunguka, ugomvi na mashindano yanazuka. Hivyo sheria haina nguvu, wala haki haitekelezwi. Waovu wanawazunguka waadilifu, hivyo hukumu hutolewa ikiwa imepotoshwa.” Mungu akasema: “Yaangalie mataifa, uone! Utastaajabu na kushangaa. Maana ninatenda kitu ukiwa bado unaishi, kitu ambacho ungeambiwa hungesadiki. Maana ninawachochea Wakaldayo, taifa lile kali na lenye hamaki! Taifa lipitalo katika nchi yote, ili kunyakua makao ya watu wengine. Wao ni watu wa kuchukiza na kutisha; wao hujiamulia wenyewe nini haki na adhama. “Farasi wao ni wepesi kuliko chui; wakali kuliko mbwamwitu wenye njaa. Wapandafarasi wao wanatoka mbali, wanaruka kasi kama tai arukiavyo mawindo. “Wote wanakuja kufanya ukatili; kwa nyuso kakamavu wanasonga mbele, wanakusanya mateka wengi kama mchanga. Wanawadhihaki wafalme, na kuwadharau watawala. Kila ngome kwao ni mzaha, wanairundikia udongo na kuiteka. Kisha wanasonga mbele kama upepo, wafanya makosa na kuwa na hatia, maana, nguvu zao ndizo mungu wao!”
Habakuki 1:1-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ufunuo aliouona nabii Habakuki. Ee BWANA, nilie hadi lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa. Mbona wanionesha uovu, na kunifanya nione mabaya? Maana uharibifu na udhalimu u mbele yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea. Kwa sababu hiyo sheria imelegea, wala hukumu haipatikani; kwa maana watu wabaya huwazunguka wenye haki; kwa sababu hiyo hukumu inayotolewa huwa imepotoshwa. Angalieni, enyi mlio kati ya mataifa, katazameni, kastaajabuni sana; kwa maana mimi natenda tendo siku zenu, ambalo hamtaliamini hata mkiambiwa. Kwa maana, angalieni, nawachochea Wakaldayo, taifa lile kali, lenye haraka kupita kiasi; wapitao katikati ya dunia, ili wayamiliki makao yasiyo yao. Hao ni watu wa kutisha sana, wa kuogofya sana; hukumu yao na ukuu wao hutoka katika nafsi zao wenyewe. Farasi wao ni wepesi kuliko chui, ni wakali kuliko mbwamwitu wa jioni; na wapanda farasi wao hujitapa naam, wapanda farasi wao watoka mbali sana; huruka kama tai afanyaye haraka ale. Wanakuja wote ili kufanya udhalimu; nyuso zao zimeelekezwa kwa bidii yao kama upepo wa mashariki, nao hukusanya mateka kama mchanga. Naam, huwadhihaki wafalme, na wakuu ni kitu cha kudharauliwa kwake; huidharau kila ngome; kwa maana huirundikia udongo, na kuitwaa. Kisha atapita kwa kasi, kama upepo, atapita na kuwa ana hatia; yeye ambaye nguvu zake ni mungu wake.
Habakuki 1:1-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ufunuo aliouona nabii Habakuki. Ee BWANA, nilie hata lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa. Mbona wanionyesha uovu, na kunitazamisha ukaidi? Maana uharibifu na udhalimu u mbele yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea. Kwa sababu hiyo sheria imelegea, wala hukumu haipatikani; kwa maana watu wabaya huwazunguka wenye haki; kwa sababu hiyo hukumu ikipatikana imepotoka. Angalieni, enyi mlio kati ya mataifa, katazameni, kastaajabuni sana; kwa maana mimi natenda tendo siku zenu, ambalo hamtaliamini hata mkiambiwa. Kwa maana, angalieni, nawaondokesha Wakaldayo, taifa lile kali, lenye haraka kupita kiasi; wapitao katikati ya dunia, ili wayamiliki makao yasiyo yao. Hao ni watu wa kutisha sana, wa kuogofya sana; hukumu yao na ukuu wao hutoka katika nafsi zao wenyewe. Farasi zao ni wepesi kuliko chui, ni wakali kuliko mbwa-mwitu wa jioni; na wapanda farasi wao hujitapa naam, wapanda farasi wao watoka mbali sana; huruka kama tai afanyaye haraka ale. Waja wote ili kufanya udhalimu; nyuso zao zimeelekezwa kwa bidii yao kama upepo wa mashariki, nao hukusanya mateka kama mchanga. Naam, huwadhihaki wafalme, na wakuu ni kitu cha kudharauliwa kwake; huidharau kila ngome; kwa maana hufanya chungu ya mavumbi, na kuitwaa. Kisha atapita kwa kasi, kama upepo, atapita na kuwa ana hatia; yeye ambaye nguvu zake ni mungu wake.
Habakuki 1:1-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Neno la unabii alilopokea nabii Habakuki. Ee BWANA, hata lini nitakuomba msaada, lakini wewe husikilizi? Au kukulilia, “Udhalimu!” lakini hutaki kuokoa? Kwa nini unanifanya nitazame dhuluma? Kwa nini unavumilia makosa? Uharibifu na udhalimu viko mbele yangu; kuna mabishano na mapambano kwa wingi. Kwa hiyo sheria imepotoshwa, nayo haki haipo kabisa. Waovu wanawazunguka wenye haki, kwa hiyo haki imepotoshwa. BWANA “Yatazame mataifa, uangalie na ushangae kabisa. Kwa sababu katika siku zako nitafanya kitu ambacho hungeamini, hata kama ungeambiwa. Tazama! Nitawainua Wakaldayo, watu wakatili na wenye haraka, ambao hupita dunia yote ili kuteka makazi yasiyo yao. Ni watu wanoogopwa na wanaotisha; wenyewe ndio sheria yao, na huinua heshima yao wenyewe. Farasi wao ni wepesi kuliko chui, na wakali kuliko mbwa-mwitu wakati wa machweo. Askari wapanda farasi wao huenda mbio; waendesha farasi wao wanatoka mbali. Wanaruka kasi kama tai ili kurarua mawindo; wote wanakuja tayari kutenda udhalimu. Makundi yao wanasonga mbele kama upepo wa jangwani, na kukusanya wafungwa kama mchanga. Wanawabeza wafalme, na kuwadhihaki watawala. Wanaicheka miji yote yenye ngome; wanalundika udongo na kuiteka hiyo miji. Kisha wanapita kasi kama upepo na kusonga mbele: watu wenye hatia, ambao nguvu zao ndio mungu wao.”