Mwanzo 9:20-29
Mwanzo 9:20-29 Biblia Habari Njema (BHN)
Noa alikuwa mkulima wa kwanza. Alilima shamba la mizabibu, akanywa divai, akalewa, kisha akalala uchi hemani mwake. Hamu, baba yake Kanaani, aliuona uchi wa baba yake, akatoka nje na kuwaambia ndugu zake wawili. Lakini Shemu na Yafethi wakatwaa nguo, wakaitanda mabegani mwao, wakaenda kinyumenyume na kuufunika uchi wa baba yao. Waliangalia pembeni, wala hawakuuona uchi wa baba yao. Noa alipolevuka na kujua alivyotendewa na mwanawe mdogo, akasema, “Kanaani na alaaniwe! Atakuwa mtumwa wa watumwa kwa ndugu zake.” Tena akasema, “Shemu na abarikiwe na Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu! Kanaani na awe mtumwa wake. Mungu na amkuze Yafethi, aishi katika hema za Shemu; Kanaani na awe mtumwa wake.” Baada ya gharika, Noa aliishi miaka 350, kisha akafariki akiwa na umri wa miaka 950.
Mwanzo 9:20-29 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao. Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea. Akasema, Na alaaniwe Kanaani; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake. Akasema, Na atukuzwe BWANA Mungu wa Shemu; Na Kanaani awe mtumwa wake. Mungu amwongezee Yafethi. Na akae katika hema za Shemu; Na Kanaani awe mtumwa wake. Na Nuhu akaishi baada ya ile gharika miaka mia tatu na hamsini. Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia tisa na hamsini, akafa.
Mwanzo 9:20-29 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao. Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea. Akasema, Na alaaniwe Kanaani; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake. Akasema, Na atukuzwe BWANA Mungu wa Shemu; Na Kanaani awe mtumwa wake. Mungu akamnafisishe Yafethi. Na akae katika hema za Shemu; Na Kanaani awe mtumwa wake. Na Nuhu akaishi baada ya ile gharika miaka mia tatu na hamsini. Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafa.
Mwanzo 9:20-29 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nuhu akawa mkulima, akawa mtu wa kwanza kupanda mizabibu. Alipokunywa huo mvinyo wake, akalewa na akalala uchi kwenye hema lake. Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake na kuwaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. Lakini Shemu na Yafethi wakachukua nguo, wakaitanda mabegani mwao wote wawili, kisha wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zilielekea upande mwingine ili wasiuone uchi wa baba yao. Nuhu alipolevuka na kujua lile mwanawe mdogo alilomtendea, akasema, “Alaaniwe Kanaani! Atakuwa mtumwa wa chini kabisa kwa ndugu zake.” Pia akasema, “Atukuzwe BWANA, Mungu wa Shemu! Kanaani na awe mtumwa wa Shemu. Mungu na apanue mipaka ya Yafethi; Yafethi na aishi katika mahema ya Shemu, na Kanaani na awe mtumwa wake.” Baada ya gharika, Nuhu aliishi miaka mia tatu na hamsini. Nuhu aliishi jumla ya miaka mia tisa na hamsini, ndipo akafa.