Mwanzo 9:18-20
Mwanzo 9:18-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Watoto wa Noa waliotoka katika safina walikuwa Shemu, Hamu na Yafethi. Hamu alikuwa baba yake Kanaani. Hao ndio watoto watatu wa Noa, na kutokana nao watu walienea duniani kote. Noa alikuwa mkulima wa kwanza. Alilima shamba la mizabibu
Mwanzo 9:18-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani. Hawa watatu walikuwa wana wa Nuhu na kwa hao nchi yote ikaenea watu. Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu
Mwanzo 9:18-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani. Hawa watatu walikuwa wana wa Nuhu na kwa hao nchi yote ikaenea watu. Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu
Mwanzo 9:18-20 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wana wa Nuhu waliotoka ndani ya safina walikuwa: Shemu, na Hamu, na Yafethi. (Hamu ndiye alikuwa baba wa Kanaani.) Hao walikuwa wana watatu wa Nuhu, na kutokana nao watu walienea katika dunia. Nuhu akawa mkulima, akawa mtu wa kwanza kupanda mizabibu.