Mwanzo 9:13-17
Mwanzo 9:13-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Naweka upinde wangu mawinguni, nao utakuwa ishara ya agano kati yangu na dunia. Kila nitakapoifunika dunia kwa mawingu, na huo upinde wa mvua utakapoonekana katika mawingu, nitalikumbuka agano langu nanyi na viumbe vyote hai. Kamwe maji hayatageuka kuwa gharika ya kuviangamiza viumbe vyote hai. Huo upinde utakapotokea mawinguni, nitauona na kulikumbuka agano hilo la milele kati yangu na viumbe vyote hai duniani.” Mungu akamwambia Noa, “Hii ndiyo ishara ya agano ambalo nimefanya na viumbe vyote hai duniani.”
Mwanzo 9:13-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi. Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni, nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili. Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi. Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na watu wote walioko katika nchi.
Mwanzo 9:13-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi. Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni, nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili. Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi. Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi.
Mwanzo 9:13-17 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nimeweka upinde wangu wa mvua mawinguni, nao utakuwa ishara ya agano nifanyalo kati yangu na dunia. Wakati wowote ninapotanda mawingu juu ya dunia na upinde wa mvua ukatokea mawinguni, nitakumbuka agano langu kati yangu na ninyi na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina. Kamwe maji hayatakuwa tena gharika ya kuangamiza uhai wote. Wakati wowote upinde wa mvua unapotokea mawinguni, nitauona na kukumbuka agano la milele kati ya Mungu na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina duniani.” Hivyo Mungu akamwambia Nuhu, “Hii ndiyo ishara ya agano ambalo nimelifanya kati yangu na viumbe vyote vilivyo hai duniani.”