Mwanzo 9:1-4
Mwanzo 9:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu akambariki Noa na wanawe, akiwaambia, “Zaeni, muongezeke, mkaijaze nchi. Wanyama wote, ndege wote wa angani, viumbe wote watambaao juu ya nchi na samaki wote wa baharini watakuwa na hofu na kuwaogopa nyinyi. Wote wamewekwa chini ya mamlaka yenu. Wanyama wote hai watakuwa chakula chenu kama vile nilivyowapa mimea kuwa chakula chenu. Lakini msile nyama yenye damu, kwani uhai uko katika damu.
Mwanzo 9:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi. Kila mnyama wa nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani: pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu. Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapa hivi vyote. Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.
Mwanzo 9:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi. Kila mnyama wa katika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani: pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu. Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote. Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.
Mwanzo 9:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndipo Mungu akawabariki Nuhu na wanawe, akiwaambia, “Zaeni, mkaongezeke kwa idadi, na mkaijaze tena dunia. Wanyama wote wa nchi, na ndege wote wa angani, na kila kiumbe kinachotambaa juu ya ardhi, na samaki wote wa baharini wamekabidhiwa mikononi mwenu, nao watawaogopa na kuwahofu. Kila kitu chenye uhai kiendacho kitakuwa chakula chenu. Kama vile nilivyowapa mimea mbalimbali, sasa nawapa kila kitu. “Lakini kamwe msile nyama ambayo bado ina damu, kwa maana damu ni uhai.